logo

NOW ON AIR

Listen in Live

“Hii kitambi yangu sasa imekuwa too much!” Sonko atangaza kutafuta gym trainer wa kike

“Jana nilitembea 3laps za 3.7kms nikahema kama punda,” Sonko alifichua.

image
na Davis Ojiambo

Burudani19 August 2024 - 11:23

Muhtasari


  • • Katika chapisho lingine, Sonko alionekana akitembea kwa miguu na kufichua kwamba alilazimika kutembea zaidi ya kilomita tatu kama njia moja ya kupunguza uzai wake.
MIKE SONKO

Mfanyibiashara na mwanasiasa Mike Sonko ameweka wazi nia yake ya kuanza safari ya kupunguza uzani wa mwili wake.

Kupitia kurasa zake katika mitandao ya kijamii, Sonko alichapisha video akitembea ndani ya gym yake na kusema kwamba anataka kuanza safari ya kupunguza uzito wa mwili wake.

Gavana huyo wa zamani wa Nairobi alisema anatafuta mkufunzi wa mazoezi ya gym wa jinsia ya kike, akisema kitambi chake kimekuwa kikubwa kupita kiasi na kuna haja yake kukipunguza kupitia mazoezi.

“Hii kitambi yangu sasa imekuwa too much. Natafuta mkufunzi wa kike wa mazoezi ya viungo kwa haraka. Mkufunzi wa mazoezi ya viungo vya kike akuje haraka upesi,” Aliandika kwenye video alizochapisha kwenye X akipapasa kitambi chake.

Katika chapisho lingine, Sonko alionekana akitembea kwa miguu na kufichua kwamba alilazimika kutembea zaidi ya kilomita tatu kama njia moja ya kupunguza uzai wake.

“Jana nilitembea 3laps za 3.7kms nikahema kama punda,” Sonko alifichua.

Hata hivyo, alisema kwamba baada ya kuweka wazi nia yake ya kuanza safari ya kupunguza uzani wa mwili, baadhi ya watu walimpa mapendekezo ya kutumia njia rahisi ya kumeza tembe za kukata uzani kuliko kuhangaika kufanya mazoezi kwenye gym.

Wengine walimshauri kufanyiwa utaratibu wa kufunga matumbo yake kama alivyofanyiwa mtangazaji Willis Raburu na balozi Big Ted.

“Sasa kuna baadhi ya marafiki wananiambia ati niende nikafanyiwe gastric bypass kama Bigted ama nifanyiwe upasuaji au nimeze puto kama Gavanaree, Raburu,” alifichua.

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved