Huenda kukawa na ushindani baina ya jamaa wawili Bradley Marongo na Isaac Otesa huku kila mmoja akidai kuwa mrefu kuliko mwingine.
Kwa wiki chache ambazo zimepita, Bradley ambaye anajulikana kama 'Gen Z Goliath' amepata umaarufu mtandaoni kutokana na urefu na ukubwa wake. Hata hivyo, Bradley hajapata kufurahia umaarufu wake kwa muda mrefu kabla ya Isaac Otesa kujitokeza na kudai kumshinda urefu.
Kwa video Isaac anasema kuwa yeye ni mrefu wa Bradley kwani yeye ana urefu wa futi 8.4 mwenzake akiwa na urefu wa futi 8.2. Anaomba kukutana na Bradley ili kuthibitisha ni nani mrefu kati yao wawili."yeye ni mfupi mimi ni mrefu...mimi natamani nifike mahali ako nione urefu wake kama ananishinda ama hanishindi"
Picha zaonyesha kufanana kati ya jitu hao wawili ila Bradley anatoka kaunti ya Vihiga na Isaac anatoka kaunti ya Bungoma.
Je, ni wazo nzuri kuwa na mashindano kati ya hao jitu wawiwli?