logo

NOW ON AIR

Listen in Live

“Asante kwa SIUUUbscribers!” CR7 avunja kimya baada ya kufikisha wafuasi 15M kwa siku

“Ahsante sana kwa SIUUUbscribers,” Ronaldo aliandika na kfichua kupeleka zawadi nyumbani

image
na Davis Ojiambo

Burudani22 August 2024 - 13:09

Muhtasari


  • • YouTube walimtunuku Ronaldo na Golden Button kwa ufanisi huo mkubwa na Ronaldo aliitaja zawadi hiyo kama ya kupeleka nyumbani kwa wanawe.
CR7

Mchezaji nguli wa Ureno na Al Nassir, Cristiano Ronaldo amevunja kimya chake saa chache baada ya kuzawadiwa na jukwaa la YouTube kufuatia mafanikio makubwa ndani ya saa chache.

Ronaldo aliarifiwa kuanzisha chaneli yake katika mtandao wa YouTube na ndani ya siku moja, tayari imepata wafuasi zaidi ya milioni 15.

YouTube walimtunuku Ronaldo na Golden Button kwa ufanisi huo mkubwa na Ronaldo aliitaja zawadi hiyo kama ya kupeleka nyumbani kwa wanawe.

Aliwashukuru wafuasi wake katika mtandao wa X na Instagram akitumia neno ‘Siuu’ ambalo ni jina la mtindo wake wa kusherehekea anapofunga bao.

“Ahsante sana kwa SIUUUbscribers,” Ronaldo aliandika na kfichua kupeleka zawadi nyumbani.

Ronaldo alificha nyumbani na kuwaita wanawe kumpokea na zawadi mpya.

“Niko na zawadi mpya, Eva njoo tucheze sisi watatu. Acha tuone nani atashinda,” Ronaldo aliwaonyesha wanawe waliopigwa na butwaa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved