Penzi linaweza kuwa tamu, lakini wakati mwingine njia za wapendanao zinaweza kuishia kwa talaka.
Mwanamuziki maarufu wa Pop na R&B, Jennifer Lopez maarufu J Lo amefanya kile ambacho kilionekana hakingetokea -- amewasilisha kesi ya talaka kutoka kwa mumewe Ben Affleck.
Hatua hiyo imesababisha gumzo kwenye mitandao baada ya kuomba kutengana na Afflick, ikimaanisha kwamba ni mwisho wa ndoa yao ya miaka miwili na kile Affleck alichowai kusema kuwa "hadithi kubwa ya wapendanao ambayo haijawai kusemwa"
Wanandoa hao wamekuwa katika ndoa kwa miaka miwili na walikuwa wanafaa kuadhimisha kumbukumbu ya ndoa siku hiyo J.Lo alipotangaza talaka.
Lopez na Afflick walibadilishana viapo Julai 16, 2022, katika kanisa la harusi la Las Vegas.
Katika ombi lake la talaka, Lopez aliorodhesha tarehe ya kutengana kuwa Aprili 26, 2024.
Jennifer Lopez ni mwigizaji, mwanamuziki, mcheza densi na mwanabiashara. Ameweza kupewa tuzo 212 kutoka kwa nafasi 341 akijumuisha tuzo tatu za American Music Awards, tuzo moja ya BET Award, tuzo moja ya Billboard Music Award, tuzo kumi za Billboard Latin Music Awards na tuzo mbili za World Music Awards.
Ben Affleck ni muigizaji na mtayarisha filamu wa Marekani ambaye ameweza kushinda tuzo mbili za Academy Awards, tuzo tatu za Golden Globe Awards, tuzo mbili za BAFTA Awards na tuzo mbili za Screen Actors Guild Awards.
Jennifer Lopez amekuwa na talaka mara tatu na hii ni ya nne, Ben akiwa kwa ya pili.
Sababu ya talaka kati ya watu hawa wawili haijulikani lakini kama msemo huenda ni milima hazikutani.