logo

NOW ON AIR

Listen in Live

“Nimepunguza kunywa pombe” Difella, jamaa anayejiita ‘Diamond wa Kenya’ akiri

Kenyan Diamond ,amesema kuwa yeye alianza usanii kutoka kitambo licha ya wakenya kumjua juzi.

image
na Davis Ojiambo

Burudani22 August 2024 - 11:19

Muhtasari


  • • Aidha, Remcy Don almaarufu Kenyan Derulo ameeleza kuwa aliongea na Jason Derulo na akamwambia kuwa ule wakati atakuwa akija Dubai ndipo wataonana.
  •  
  • • Vile vile, wamesema kuwa wako na kitu kipya ambacho wanazidi kukipika pamoja na wanaamini kuwa watu watakipenda kutokana na wao kuwa na talanta .
Jason Derulo na Diamond feki

Difella Music, Mkenya anayetamba kuwa anamfanana gwiji wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amefichua kwamba amepunguza unywaji wa pombe.

Kupitia video walipokuwa wakihojiwa Diamo nd feki alieleza kuwa amebadilisha maisha ambayo alikwa akiishi baada ya kuwa na umaarufu.

"Nimepunguza pombe juu kutoka nikuwe famous,nikiingia mahali labda nikunywe 20k juu ya kununulia watu", alisema.

Aidha, Remcy Don almaarufu Kenyan Derulo ameeleza kuwa aliongea na Jason Derulo na akamwambia kuwa ule wakati atakuwa akija Dubai ndipo wataonana.

Aidha kenyan Diamond amesema kuwa yeye ni mchapakazi katika tasnia ya muziki na angependa Diamond Platinumz kumtambua katika kazi yake anayohifanya.

Vile vile, wamesema kuwa wako na kitu kipya ambacho wanazidi kukipika pamoja na wanaamini kuwa watu watakipenda kutokana na wao kuwa na talanta .

Kenyan Diamond ,amesema kuwa yeye alianza usanii kutoka kitambo licha ya wakenya kumjua baada ya video waliofanya na Remcy Don.

Aidha Remcy amesema hapo awali akuwa na hela za kutolesha video lakini kwa sasa yuko vizuri na kwasasa ametolesha ngoma yake iliyokosti 600k pesa za Kenya.

Remcy ameelezea kuwa alipitia changamoto ili kumfikia Jason Derulo lakini sasa wanajuana na Remcy yuko tayari wafanywe collabo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved