logo

NOW ON AIR

Listen in Live

MP Salasya aonyesha mchoro wa nyumba yake itakayojengwa

salasya anatarajiwa kujenga jumba la mamilioni mtaa wa kijiji cha kisumundogo alikozaliwa.

image
na Davis Ojiambo

Burudani23 August 2024 - 09:59

Muhtasari


  • •Mp Salasya aonyesha mchoro wa nyumba ambayo amewazia kujenga kijijini akisema kuwa hawezi kuwa na nyumba nzuri Mjini kuliko kijijini alikozaliwa mtaa wa Kisumundogo.Ni jambo ambalo wafuasi wako wamelikubali na kumpongeza kwa bidii yake kijendeleza.
PK SALASYA

Mbunge wa Mumias Mashariki Peter Selasya ambaye huvutia wafuasi wengi kutokana na ucheshi wake ,sasa ameonyesha mchoro wa jumba ambalo amewazia kujenga kijijini  maoneo ya Kisumundogo.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook PK amesema kuwa maono yake ni kujenga jumba ambalo ametoa mchoro  wake pale nyumbani ambako ndiko chimbuko lake.

"Nyumbani ni kwema kila wakati,na pendelea kujenga nyumba kijijini  pale Kisumundogo Mumias East lakini si Nairobi.Wakati unajenga nyumba katika kijiji,'ancestors' wanafurahia,siwezi kuwa na nyumba nzuri Nairobi kushinda kijijini,na hili ndilo litakuwa jumba pale Mumias East,Mungu akijaalia", alisema.

Ikumbukwe ni siku chache baada ya PK kutangaza kuwa anatafuta mwanadada ambaye atakuwa akimpikia licha yake kuchoka kupikiwa na wanaume ugali kwa sukuma kwa mujibu wa alichosema,"Nimechoka kupikiwa ugali na sukuma kila siku na wanaume wezangu " .

Kutokana na posti hiyo baadhi ya wafuasi wake walionekana kufurahishwa na wazo hilo huku nwengi wafanya mzaha na kusema kuwa ni jirani yake atakuwa akimtembelea "eeeeeiii nitakuwa nakutembelea kila wikendi kukuletea matunda na mboga za majani,harakisha" mfuasi alisema,Vile vile vijana wenzake hawakuachwa nyuma huku wakisema "eeei hapa itabidi vijana wewe nana room ya mzinga hapo rooftop"...alisema kwa utani .


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved