Mwimbaji na mjasiriamali maarufu wa Kenya Esther Akoth almaarufu Akothee ameibua wasiwasi kuhusu baadhi ya watu anaowakaribisha maishani mwake.
Katika taarifa fupi ya Alhamisi usiku, mama huyo wa watoto watano alilalamika kwamba hapo awali amekubali hata watu wasiomtakia mema.
Kufuatia hayo, aliuliza kibalagha kuhusu jinsi ya kufuta moyo wake akibainisha kuwa umekuwa ukimdanganya kila mara.
“Nawezaje kuufuta moyo wangu? Unaendelea kunidanganya, unakubali hata wale wanaotamani kuniona nimekufa. Tafadhali, ninawezaje kufuta moyo wangu?,” Akothee alihoji kupitia Instastori zake.
Hata hivyo, hakutoa maelezo zaidi kuhusu kwa nini alitoa taarifa hiyo ya kimafumbo.
Haya yanajiri wiki moja tu baada ya mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 43 kurejea nchini kutoka Uganda ambako alidai kufanya viapo upya na mpenzi wake, Nelly Oaks.
Katika chapisho la Jumatatu wiki jana, msanii huyo alitoa shukrani zake kwa nchi hiyo jirani akikiri kwamba mapenzi yao yaliimarishwa huko.
“Yooo Uganda walituharibu, tulienda kama meneja na msanii, tunarudi nyumbani kama mke na mume. Je, Uliona viapo vyetu vikifanywa upya Uganda? Asante sana Uganda, umeimarisha maisha yangu ya Upendo. Nakupenda Uganda,” aliandika.
Wawili hao ambao pamoja na kuwa wapenzi, pia ni washirika wa kikazi walikuwa katika safari inayohusiana na utalii nchini Uganda.
Katika ziara yao, walipata nafasi ya kuzuru maeneo kadhaa ya nchi hiyo jirani, kukutana na watu mashuhuri pamoja na mashabiki.
Katika mojawapo ya machapisho yake ya matangazo, mama huyo wa watoto watano alidai kuwa mpenzi wake anataka angalau watoto wanne, huku mmoja akiitwa Elizabeth Uganda Okuna.
“Yooo Uganda, Tumefanya upya viapo vyetu tayari. Ardhi ya mahaba na utulivu. Ona hewa safi za ndege,” Akothee aliandika chini ya picha zake na Nelly Oaks alizochapisha Ijumaa,
Aliongeza, "Nelly anaomba watoto 4 na badomtoto nambari moja ni kupanda tu 🤣🤣🤣🤣🤣. Nelly anasema mtoto wake ataitwa Elizabeth Uganda Okuna 🇺🇬. Yawaaa.”
Wawili hao wamekuwa wakichumbiana kwa muda mrefu sasa, hata hivyo wameachana na kurudiana mara kadhaa.