Mwanahabari maarufu wa Uganda ajibu baada ya kupendekezwa kuwa mwenyekiti wa AU

Katika majibu yake, mwanahabari huyo aliyeonekana kushangazwa alisema, "Katika mabadiliko ya matukio ..."

Muhtasari

•Bw Njala alionekana kushangazwa sana baada ya kura ya maoni kufanywa kukusanya maoni kuhusu yeye kuwa mwenyekiti ajaye wa Umoja wa Afrika.

•Wengi waliotoa maoni walionekana kuunga mkono wazo hilo huku baadhi wakibainisha kuwa yeye ni mwaminifu siku zote.

Simon Kaggwa Njala
Mwanahabari Simon Kaggwa Njala
Image: HISANI

Mwanahabari maarufu nwa Uganda Simon Kaggwa Njala alionekana kushangazwa sana baada ya kura ya maoni ya mitandaoni kufanywa kukusanya maoni kuhusu yeye kuwa mwenyekiti ajaye wa Umoja wa Afrika.

Akaunti ya Twitter, Africa Archives, ilifanya kura ya maoni ikiwauliza watumiaji wa mtandao kama wanamuunga mkono mwanahabari huyo mcheshi kuchukua nafasi hiyo kubwa ya bara.

"Je, unamuunga mkono mtu huyu kutoka Uganda kuwa mwenyekiti wa Umoja wa Afrika?" kura ya maoni kwenye akaunti ya African Archives ilisoma.

Katika majibu yake, mwandishi wa habari huyo aliyeonekana kushangazwa alisema, "Katika mabadiliko ya matukio ..."

Wanamtandao wengi waliotoa maoni chini ya kura hiyo ya maoni walionekana kuunga mkono wazo hilo huku baadhi wakibainisha kuwa yeye ni mwaminifu siku zote.

Tazama majibu ya baadhi ya watumiaji wa mtandao:

@AravindBarca: Anazungumza ukweli, kwa nini isiwe?

@iam_igumira: Ninamuunga mkono kikamilifu. Ana sifa zote za kuwa kiongozi.

@_ValentinoXO: Ana kura yangu.

@elanbehh: Inategemea na sifa zake na maono ya jukumu hilo. Asili yake ni nini?

@EliasOO1L: Hiyo inamaanisha hakuna LGBTQI barani Afrika.

Image: X

Bw Simon Kaggwa Njala alipata umaarufu miaka kadhaa iliyopita baada ya mahojiano yake ya awali na mwanaharakati wa Uganda Pepe Julian Onziema kusambaa mitandaoni.

Mwaka jana, mwanahabari huyo aliyefanya mahojiano yaliyovuma ya ‘Why are you gay?’ zaidi ya muongo mmoja uliopita alikiri kuchoshwa na watu wanaoibua upya video ya mahojiano hayo yenye utata kila kukicha.

Mwaka wa 2012, mwanahabari Simon Kaggwa Njala alimhoji mwanaharakati wa haki za wapenzi wa jinsia moja nchini Uganda,  Pepe Julian Onziema katika kipindi chake cha Morning Breeze kwenye steseheni ya CBS TV na tangu wakati huo mahojiano hayo yamekuwa yakivunja mbavu za wengi kote ulimwenguni kutokana na jinsi alivyoyaendesha wa njia ya ucheshi.

Mtumizi mmoja wa mitandao alitengeneza video ya katuni ya mahojiano hayo mwaka jana na kuichapishwa kwenye mtandao wa Twitter akimsifu mwanahabari huyo kwa jinsi alivyofanya mahojiano hayo.

"Forever goated @SimonKaggwaNjal," mtumiaji wa Twitter kwa jina @Abrahamlyon1 aliandika chini ya video hiyo.

Bw Kaggwa hata hivyo alionekana kutopenda wazo la mahojiano hayo kufufuliwa upya na akajibu, “Dear Lord, When will this interview rest?”

Kumaanisha: Mungu Mpendwa, Mahojiano haya yatapumzika lini?

Haikuwa mara ya kwanza kwa mwanahabari huyo wa Uganda kulalamika kuhusu mahojiano aliyofanya muongo mmoja uliopita kurejeshwa.

Mwaka wa 2022, akaunti ya Twitter @AfricaFactsZone ilichapisha klipu fupi ya mahojiano hayo na kuyataja kama mahojiano maarufu zaidi nchini Uganda.

"Mahojiano maarufu zaidi nchini Uganda. Mwandishi wa habari anauliza mtu kuhusu jinsia yake," maelezo ya video hiyo yalisoma.

Kaggwa ambaye alionekana kuchoshwa na video hiyo kuzungumziwa mara kwa mara alijibu, "Lakini kusema kweli, hii ilikuwa miaka kumi iliyopita! Boy child  ameteseka. "

Jibu la mwanahabari huyo lilidokeza kwamba mahojiano hayo huenda yalimletea matatizo fulani yasiyojulikana.