Wasanii hao wawili wamekuwa wakimenyana kwa muda mrefu, kila mmoja akiwa na kundi lake la mashabiki wanaoamini kwamba mshua wao ndiye msanii bora zaidi wa miziki ya Afrobeats kuwahi kutkea.
Hata hivyo, katika video ya hivi majuzi, Cristiano Ronaldo alionekana kumaliza kabisa mjadala huo, akimtaja msanii bora kati ya hao wawili.
Video hiyo iliibuka mtandaoni wiki kadhaa baada ya mwanasoka huyo bora wa dunia mara 5 kuwafanya Wanigeria kushangilia huku akisikiza wimbo wa Asake "Active" akimshirikisha rapa wa Kimarekani Travis Scott kutoka kwenye albamu ya Lungu.
Inafahamika kuwa mchuano kati ya Wizkid na Davido umekuwa mrefu zaidi katika tasnia ya burudani nchini Nigeria kwani mashabiki wa waimbaji hao huwa wanapigana wenyewe kuhusu nani bora kati ya waimbaji hao wawili.
Hata hivyo, wakati akitengeneza maudhui kwenye ukurasa wake wa YouTube, Cristiano Ronaldo aliombwa kuchagua bora kati ya Wizkid na Davido na hakupoteza muda kutoa jibu lake la uaminifu.
Katika klipu hiyo, Crisitiano Ronaldo mwenye umri wa miaka 39 ambaye anacheza na Al-Nasr nchini Saudi Arabia anamchagua mwimbaji nyota wa Afrobeats Davido kama mwimbaji anayempenda zaidi mbele ya mshindi wa tuzo ya Grammy Wizkid.
Uchunguzi wa haraka ulithibitisha kuwa Cristiano Ronaldo na Davido wana urafiki mkubwa kwenye Instagram, hata hivyo Cristiano Ronaldo na Wizkid hawafuatikani. Wizkid hafuati mtu yeyote kwenye Instagram.