Msanii Harmonize, amefahamika na wengi wa mashabiki wake kama mtu anayependa warembo wazuri na wenye wamebarikiwa na viuno vipana.
Katika wimbo wake wa hivi karibuni aliofanya na Nandy, mrembo huyo ambaye ni mke wa Billnass alimtia katika majaribu kwa kutokea na vazi lililombana kiasi kwamba lilidhihirisha maungo yake.
Katika wimbo huo ‘usemi sina’ Harmonize na Nandy waliigiza kama wapenzi lakini katika muda wote, wakalinda mipaka ya heshima yao, Harmonize akiweka akilini kwamba Nandy ni mke wa mtu.
Hata hivyo, kwa jinsi Nandy alivyotokea kwenye video kuliibua maswali kwa baadhi ya mashabiki ambao walilenga kujua kama Harmonize aligusa ili kuthibitisha.
Akionekana kuwajibu mashabiki hao, Harmonize alisema kwamba hata yeye hana uhakika kama Nandy alikuwa na umbile la kweli au aliongeza na kigodoro juu.
Alijitetea akisema kwamba katika muda wote wa ngoma, alimheshimu kama shemeji yake na ndio maana asingetaka kujiletea skendo kwa kumtaguza katika sehemu kama hizo.
“Swala la kusema Nandy Alivaa kigodoro 😂😂 Kiukweli mimi Sina Uhakika Nalo maana Ukishoot na Shemeji Sharti la kwanza Hutakiwi kumgusa,” Harmonize alisema.
“Baadhi ya maeneo Nyeti kama hayo !!! Binafsi Nimejionea Tu BOMBO CLAAATY !!😂 Mashine ni mashine !!😂 Kwani Mmeona nini ?? Minong’ono ni mingi Ngoja niangalie Tena Nikiwa nishavuta Hivi narudia,” aliongeza kwa utani.
Katika kipindi cha wiki moja iliyopita, Harmonize na Nandy wameachia ngoma mbili za mapenzi, wakiimba kwa usanjari wa kipekee utadhani ni mtu na mpenzi wake.
Hata hivyo, Harmonize aliyekiri kuvutiwa na wanadada wenye viuno vinene aliomba kukutanishwa na mzee mmoja aliyekiri kwamba alifilisika kutokana na hulka yake ya kuwapenda warembo ‘waliobeba