logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Tukiamka mapema twende wapi? - Tom Daktari auliza.

Kulingana naye, matajiri wana sababu za kuamka mapema tofauti sana na wale ambao hawajabarikiwa kimfuko.

image
na KEZIA ACHIENG'

Burudani31 October 2024 - 15:18

Muhtasari



  • Imekuwa msemo kwa muda mrefu kuwa matajiri hawalali kwa masaa 8 na kwamba ukipenda kulala hutakuwa tajiri.
Tom Daktari aliingilia kati na kutetea wale ambao sio matajiri (yeye akiwa mmoja wao) na kuuliza wanatakiwa kwenda wapi baada ya kuamka.
Kulingana naye, matajiri wana sababu za kuamka mapema tofauti sana na wale ambao hawajabarikiwa kimfuko.

“Ati ooh unalala sana hivo utakuwa tajiri kweli. Ati ooh rich people do not sleep 8 hours a day alafu mnaachia hapo. Hamtuambii sisi tukiamka mapema tunafaa kuenda wapi. Hamtuambii tukishaamka 4:00 asubuhi utajiri inaingia aje hamtuambii mnatuwacha hapo kwa kuamka. Infact unafaa utuambie tukiamka mapema tunapigia nani. Kwani tajiri atalala aje sana na ako na pesa anafaa kuendea?. Mimi naye nitalala, nitalala hadi niamshwe na mbu,”


“Tukiamka mapema twende wapi?” Daktari aliuliza.


Kwenye posti nyingine, Daktari alisimulia jinsi mtu anaweza kosa bahati.


Kuna aina tofauti ya watu katika kampuni, yule ambaye hutia bidii kazini na yule ambaye huchelewa kufika kazini na ni mvivu.


Cha kushangaza ni kuwa, yule ambaye ni mvivu ndiye huongezewa mshahara na hata kupandishwa cheo wakati yule mwenye bidii hufutwa kazi.


“Unatia bidii kazini ndio kampuni iende next level, sazingine hata lunch huendi, unatoka late hours wewe sasa ndio wanafuta, wewe ndio wa kufuta. Yule mwenye anakuja late ako tu anakaa lazy, huyo ndio wanaongezea mshahara huyo kwanza anapewa cheo anakuwa mkubwa wako,”


Daktari anaendelea na kusema kwamba alikuwa na rafiki kama huyo na siku moja alimuuliza siri yake ni nini. Rafiki yake alimwambia awache kufanya kazi kwa bidii, afanye kazi kwa busara.


“Mimi nilikuwa na collegue kama huyo lakini sekta yangu iko chini kuliko yake nikamuuliza siri ni nini? Akaniambia bro stop working hard work smart. Kumbe huyu jamaa akishachoka, yeye hupiga kabreak kidogo alafu anaendelea mimi nikiwa namastress bado niko kazi sasa itaendelea aje?”


“Haya maisha unaweza kuwa unlucky ushangae,” aliandika.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved