Muigizaji wa muda mrefu wa filamu za Kiswahili kutoka Tanzania, Grace Mapunda ameripotiwa kufariki dunia.
Haya ni kwa mujibu wa waigizaji wenzake katika mitandao mbalimbali ya kijamii.
Jiffy Pictures yake Lulu Hassan pia imetoa taarifa hizo ikimumboleza kama mtu aliyejitolea katikakazi yakevya uigizaji.
Mpaka kufariki kwake, Mapunda alikuwa anaigiza kama Tesa kwenye kipindi cha Huba ambacho kinazalishwa na Jiffy Pictures ya Lulu Hassan na Rashid Abdalla kwenye Maisha Magic Bongo.
“Tumeondokewa Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na Kwake ni marejeo,Kwaniaba ya Familia ya Grace mapunda tunawajulisha kua Mama yetu Mpendwa Grace Mapunda (TESA) hutupo nae tena Duniani,Bwana ametoa,Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe,” Jiffy Pictures walitoa sasisho kupitia ukurasa wao wa Facebook asubuhi ya Novemba 2.
Taarifa mbalimbali zinadai kwamba Mapunda alifariki hospitalini baada ya kulazwa kwa muda mfupi ambapo alilazwa Novemba 1.
Grace Mapunda atakumbukwa kwa mchango wake kwenye sekta ya maigizo, akicheza kama Mama mzazi wa mastaa wengi.