Mwimbaji nyota wa Nigeria, Davido ametoa tathmini yake ya kikweli kuhusu jinsi muziki wa Afrobeats umekua barani Afrika na nje ya bara.
Akizungumza na Kiss Fress UK, Davido alisema kwamba ni kupitia wasanii wa kizazi chake ambapo muziki wa Afrobeats uliweza kukua na kujivutia umaarufu ndani ya nje ya Afrika.
Alisema kwamba athari ya muziki huo ni kubwa kiasi kwamba nje ya Afrika, kila mtu anajua muziki wa Afrika nzima unaitwa Afrobeats hali ya kuwa ni mdundo tu unaohusishwa na mataifa ya Afrika Magharibi.
Davido alisema kwamba imefikia kiwango kwamba hata wasanii kutoka Marekani wanataka kujihusisha na Afrobeats kutokana na athari chanya ya muziki huo.
"Msimu huu wa kiangazi, nilikuwa Ulaya sana… niliona kwamba mazingira yamebadilika. Watu wanapenda Afrobeats. Hata wasanii wa Marekani wanataka kufanya Afrobeats badala ya sauti zao wenyewe,” alisisitiza
Alisisitiza kuwa ushawishi wa kitamaduni unaoongezeka wa Afrika unaenea zaidi ya muziki, akisema, "Sasa, masimulizi [kuhusu Waafrika] yamebadilika. Heshima ipo, sio tu kwenye muziki bali kwenye mitindo, chakula.”
Muziki wa Afrobeats umekuwa ukijulikana kama ni sauti jumuishi ya miziki ya Afrika, dhana ambapo wasanii wengine haswa kutoka Afrika Kusini wamekuwa wakipinga vikali.
Kwa mujibu wa sanii kutoka Afrika ya Kusini, Afrobeatz ni midundo ya Afrika Maghharibi tu na wao wana sauti yao kwa kina Amapiano.
MSHINDI WA Grammy, Tyla alizua dhana hiyo miezi michache iliyopita aliposhinda tuzo ya MTV kama msanii bora wa Afrobeats na wimbo wake wa ‘Waters’ na kusema kwamba japo alishinda, lakini kitengo alichoshinda si sahihi akisisitiza yeye si msanii wa Afrobeats bali Amapiano.