Cassypool amemshauri mchekeshaji aliyegeuka kuwa mwanaharakati, Eric Omondi kumgeukia Mungu.
Akizungumza na waandishi wa habari za burudani baada ya kuwasili nchini kutoka Uarabuni alikokaa kwa siku kadhaa, Cassypool alimtaka Omondi kuchukua muda na kujitathmini, kwa kuangazia kisa cha Gachagua.
Cassypool alimshauri Eric kuacha kujikita sana kwa watu bali kujita uhusiano wake kwa Mungu, akisema kwamba watu wanakusifia leo lakini kesho watakugeuzia mkuki.
“Nataka kuambia Eric Omondi, hawa binadamu ambapo unasema sisi, wanajipendekeza, nataka kukusisitizia kwa kukuambia kitu kimoja; binadamu bila Mungu kuwashika roho, watakugeuka,” Cassypool alisema.
“Wao wenye wanakupigia makofi kesho watakucheka na kusema wewe umefeli. Fanya kutafuta uso wa mwenyezi Mungu, chunga na kuheshimu watoto wako maana urafiki na umaarufu huisha,’ Cassypool aliongeza.
Alitolea mfano wa aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua jinsi amebadilika na kuwa mwananchi wa Kawaida ndani ya siku chache tu.
“Nani angejua kwamba naibu wa rais atakuwa mtu wa kawaida tutakuwa tunapiga na yeye stori? Sasa hivi tukikutana naye nitamsalimia kwa kichwa na kila mtu anaenda zake. Kwa sababu hana kirauni kwa kichwa lakini tukiona Kindiki tutasimama na kumpigia saluti kwa sababu ndiye DP sasa,” Cassypool alisema.
Aliwasisitizia watu kuhakikisha uhusiano wao na Mungu upo imara, akisema urafiki hufika mahali unaisha. “Heshimu Mungu, urafiki unaisha.
Hivi vitu ambavyio tunatafuta sasa hivi vitaisha, watu ambao walikuwa na majina makubwa wapo kwenye makaburi wamelala.
Mbona wasijitoe pale kwa makaburi? Mbona pesa zao zisiwaokoe?” Cassypool alihoji.