logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Salasya afurahi kuona picha yake kwenye gari Murang’a licha ya yeye kutoka Magharibi

“Eshienyu ni eshienyu katika luhya ina maana chenu ni chenu ata kikiwa kibaya (ninasherehekewa na kuthaminiwa sana hapa Kenya)," alisema.

image
na MOSES SAGWEjournalist

Burudani06 November 2024 - 15:37

Muhtasari


  • Mbunge huyo alipata umaarufu wa kisiasa baada ya kushinda kiti cha ubunge chini ya chama cha Democratic Action Party of Kenya (DAP-K) mnamo 2022.



Mbunge wa Mumias Mashariki, Peter Salasya ameonyesha furaha yake baada ya kuona picha yake ikiwa kwenye gari moja la abiria katika kaunti ya Murang’a.

Akionyesha furaha yake kupitia Instagram, Mbunge huyo mcheshi alisema kwamba jina lake kuonekana kwenye gari ni neema ya kipekee si tu kwake bali pia kwa wanaolitumia kwa usafiri na mwenye gari pia.

Aliwarai watu kuweka picha zake kwenye magari yao akidai kwamba hiyo ndio njia ya kujipatia Baraka na neema.

“Matatu hii ilionekana Murang’a, nina furaha sana. Ukiona gari lolote lililoandikwa hivi hata kama uko na gari lako tu kupanda na kuhama kwa kilomita chache na kulipa ili kupokea neema. Waah, Navuma zaidi hapa Kenya watoto wetu na hata katika ardhi ya Kikuyu."

Alitumia fursa hiyo kuwashauri watu haswa kutoka kwao Magharibi mwa Kenya kuwa na mazoea ya kukumbatia na kusherehekea mtu wao hata kama ni mbaya kuliko kuacha watu wa nje kuwaonyesha njia.

“ Eshienyu ni eshienyu katika luhya ina maana chenu ni chenu ata kikiwa kibaya (ninasherehekewa na kuthaminiwa sana hapa Kenya)," alisema.

Mbunge huyo alipata umaarufu wa kisiasa baada ya kushinda kiti cha ubunge chini ya chama cha Democratic Action Party of Kenya (DAP-K) mnamo 2022.

Hivi majuzi alishiriki hadithi kuhusu mwanzo wake mnyenyekevu. Mnamo Agosti 10, 2024, mbunge huyo alichapisha picha ya nyumba ya kawaida ambayo alisema ni ya mamake na ndugu zake pacha miaka miwili tu iliyopita, kabla ya kujipatia umaarufu wa kisiasa.

Katika chapisho lake, Salasya alishiriki kwamba hali yake ya maisha ilikuwa ngumu sana wakati huo.

Nyumba yake ilikosa huduma za kimsingi kama vile madirisha na uingizaji hewa mzuri, na hakuwa na hata kitanda, mara nyingi akilala sakafuni.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved