Mwanamuziki wa Tanzania Harmonize amekiri kuwa anataka
kuingia kwenye mahusiano na mwanamke ambaye ana imani ya dini ya Kiislamu na
wala si Mkiristo.
Msanii huyo amefichua hayo Jumanne mchana kwenye ukurasa
wake wa Instagram ambapo amesema kuwa wasichana wa Kikristo ndio wanavutiwa zaidi
naye.
Harmonize amesema kuwa amegundua kwamba katika maisha yake,
hajawai kuwa na mahusiano ya kweli na binti wa Kiislamu .
“Yani leo ndio nimegundua sijawahi kuwa in serious relationship na
binti yeyote wa Kiislamu maisha yangu yote!!!” Alisema Harmonize.
Msanii huyo anayemiliki lebo ya Konde Music Worldwide anaamini
kuwa huenda mwanamke atakayemwoa anatoka dini ya Kiislamu akitaka mashabiki
kumsaidia kupata msichana wa Kisslamu anayeweza kuingia kwenye mahusiano naye.
Msanii huyo amekuwa kwenye mahusiano kadhaa wa kadhaa yote
yakiishia kuvunjika kabla ya kuingia rasmi kwenye ndoa.
Mwezi Oktoba, Rajab Abdul Kahali maarufu kama Harmonize
alidhibitisha kuwachana na mpenzi wake ambaye ni shoshalaiti Poshy Queen akisema
kwamba kile alichoweka wazi kwa umma lazima atangaze kuwa wamewachana kwa umma
vile vile.
Kabla ya kuwa kwenye uhusiano wa mapenzina Poshy Queen, msanii
huyo awali alikuwa kwenye mahusiano na Kajala ambapo pia mahaba hayo
hayakudumu.
Ila, Harmonize ametoa sharti kuwa lazima msichana
wa Kiislamu atakayempata awe amefungasha mashine.