Mwanamuziki wa Bongo Zuchu ametangaza kutengana na mpenzi
wake ambaye pia ni mwanamuziki wa Tanzania Diamond Platnumz baada ya kuwa
kwenye mahusiano kwa mujda wa miaka mitatu.
Kwa mujibu wa Zuchu, kupitia taarifa aliyoichapisha kwenye
ukurasa wa Instagram, amesema kuwa yeye na Diamond wamekubaliana kukatisha
mahaba baina yao.
Tangazo hili linajiri wiki chache baada ya Zuchu kumwambia
Naseeb Abdul Juma maarufu kama Diamond Platnumz kuwa hatakubali kumzalia hadi
wakati ambapo atamwoa kikamilifu.
Katika hafla moja ya burudani iliyowaleta pamoja wasanii hao
wawili, Diamond alimuuliza Zuchu ikiwa anamwamini ili angalau amzalie mtoto ila
Zuchu alimpa masharti ambayo angemzalia Diamond ikiwa angeyatekeleza.
“Unanipenda. Unanitaka. Tanioa lini? Hapo ndipo nitakuzalia.” Alijibu Zuchu.
Katika ujumbe wa Zuchu akitangaza kuwachana na Simba, aidha
amesema kuwa kuna kazi ambayo anaifanya na Diamond akiwataka mashabiki
wasishangae kazi hiyo ikiwachiliwa.
Vile vile mwimbaji huyo wa kibao cha Utaniua amemtakia
Diamond kila la heri akisema kuwa malengo yake kwa sasa ni kupata nafuu kutokana
na kuvunjika kwa mahusiano yao. Pia, Zuchu amewaomba mashabiki kumpa sapoti
katika taaluma yake ya muziki wakati huu moyo unavuja.
Katika chapisho lake la Jumanne mchana, Zuchu amefunga sehemu ya mashabiki kutoa maoni yao kwenye chapisho lake.
Diamond Platnumz pia amechapicha ujumbe wa Zuchu kwenye ukurasa wake wa Instagram bila ya kusema lolote.