Bradley Marongo, maarufu kama Gen Z Goliath
amewashangaza mashabiki wake wengi baada ya kumtambulisha mpenzi wake mpya.
Jamaa huo anayejinadi kama mwanadamu mrefu zaidi
nchini Kenya alitetea uamuzi wake akisema kwamba mapenzi hayatambui kabila,
mipaka wala rangi ya ngozi.
Alimtambulisha mrembo kutoka Ujerumani kama mpenzi
wake na kusema kwamba pamoja watakuwa wanafunzana na kubadilishana utamaduni
lakini pia kuweka historia ya kipekee katika maisha yao.
“Mapenzi
hayajui mipaka, ninawaleteeni mpenzi
wangu mpya kutoka Ujerumani kwa watu wangu wa ajabu wa Kenya. Hapa tunabadilishana
na kuwianisha utamaduni lakini pia kutengeneza kumbukumbu pamoja,”
Bradley Mtall aliandika.
Tangazo hili linajiri miezi michache baada ya Marongo
kuweka wazi uvumi kuwa alikuwa na mke na kumtelekeza nyumbani kijijini baada ya
kupata umaarufu.
Madai hayo yaliibuliwa miezi kadhaa iliyopita
alipopata umaarufu na fulusi ambapo mama yake alikuwa wa kwanza kudai kuwa
mwanaye amebadilika na hata hawatazami nyumbani.
Hata hivo, akijibu, Bradley alinyoosha maelezo kwamba
tatizo kuu ya mama yake ilikuwa kwamba alitaka kila mahali alikokwenda waende
na yeye, jambo ambalo alisema halingewezekana.
Marongo alisema kwamba hajaisahau na hawezi kuisahau
familia yake, akifichua kuwa alikuwa amemtumia mama yake hela.
Kuhusu mwanamke aliyedaiwa kuwa mpenzi wake, Marongo
alisema kuwa hakuwahi muoa na kwamba mrembo huyo alikuwa amemuacha kutokana na
ugumu wa maisha.
Jamaa huyo mrefu alimwaga mtama zaidi akisema kuwa
mwanamke huyo alianza kujibebisha kwake baada ya umaarufu na fulusi kutua
kwake, akimtuhumu kwa kutaka kushusha kitonga kwake na kuteleza kwa ganda la
ndizi kimaisha.