logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Diana Marua aandika barua kali ya motisha kwa mwanawe wa kulea Morgan Bahati

Diana alimueleza mwanawe jinsi ulimwengu ulivyo mgumu na kumwambia kuhusu mambo ya kutarajia maishani.

image
na Samuel Mainajournalist

Burudani19 November 2024 - 10:42

Muhtasari


  • Diana mnamo Jumapili alimwandikia mwanawe wa kulea Morgan Bahati ujumbe mzuri wa motisha kupitia akaunti yake ya Instagram.
  • Diana pia alimhakikishia Morgan kuhusu upendo wake mkubwa kwake.


Mtayarishaji maudhui Diana Marua mnamo Jumapili alimwandikia mwanawe wa kulea Morgan Bahati ujumbe mzuri wa motisha kupitia akaunti yake ya Instagram.

Katika barua yake, Diana alimueleza mwanawe jinsi ulimwengu ulivyo mgumu na kumwambia kuhusu mambo ya kutarajia maishani.

Pia alitumia fursa hiyo kumshauri kijana huyo wa miaka 14 jinsi ya kukabiliana na changamoto za maisha.

"Mpendwa Morgan, ulimwengu ni mahali pa ukatili. Hata hivyo, katika ukatili wake, ni mahali ambapo Mungu aliumba kwa ajili yetu sote. Ni juu yako na mimi kuifanya sehemu ndogo ya Mbingu kwa ajili yetu na watu muhimu,” Diana Marua alimwandikia mwanawe.

Aliongeza, "Utakumbana na Majaribu mengi, Changamoto, hali duni lakini katika hayo yote, utashinda hata iweje. Katika maisha, kila wakati Chukua masomo na uyaweke moyoni mwako.”

Mama huyo wa watoto watatu pia alizungumza juu ya maono makubwa aliyonayo kwa mtoto huyo wake wa kule na akamhakikishia sapoti yake.

"Jambo moja najua, utakuwa na familia nzuri na yenye mafanikio. Umeona jinsi baba yako anavyonipenda bila masharti. Tumezungumza kuhusu mipango yako ya siku za usoni na kwa uaminifu, ndoto zako zinanipa tabu,” alisema.

"Umekusudiwa ukuu, na mimi na Baba tuko hapa kukuunga mkono hadi mbawa zetu zianguka. Wewe ni Baraka yetu Kubwa na tukulee kulingana na mapenzi ya Mungu πŸ™,” aliongeza.

Diana pia alimhakikishia Morgan kuhusu upendo wake mkubwa kwake.

Morgan ni mtoto wa kulea wa Bahati na Diana Marua, na ndiye mtoto mkubwa zaidi katika familia yao.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logoΒ© Radio Jambo 2024. All rights reserved