RAPA na mtengeneza maudhui, Diana Marua amemshauri
binti yake mzaliwa wa kwanza, Heaven Bahati umuhimu wa kuzaa watoto angalau 5.
Akizungumza naye wakati walikuwa kwenye ziara ya mama
na binti ndani ya gari lao, Diana Marua alilenga kujua maazimio ya binti yake
kuhusu familia katika maisha yake ya baadae.
Binti huyo alisema kwamba angependa kuzaa watoto 5
lakini akasema kwamba atafurahi zaidi iwapo atapata 2 tu.
Mtoto huyo alisema kwamba anachagua 2 kwa sababu
watamrahisishia kazi ya malezi, jambo ambalo mamake alimtaka kufikisha 5 akimpa
hakikisho la kumsaidia katika malezi.
“Mimi
nataka kupata watoto 5 kama wewe,” Heaven Bahati
alimwambia mamake mwanzoni.
“Nikikua
mtu mzima ningependa lakini kuwa na watoto 2 tu. Kwa sababu sitaki kulea watoto
wengi. Kulea watoto wengi ni kazi ngumu,” mtoto huyo
alibadili msimamo wake baada ya mamake kumuuliza sababu ya kutaka watoto.
Baada ya kusisitiza, akiambatanisha na sababu za
kutaka watoto 2 pekee, Diana Marua alimshauri bintiye kwa kumbembeleza kupata
watoto 5 angalau.
Marua alimwambia bintiye kwamba kupata watoto 5 ni vizuri,
akimhakikishia kwamba atakuwa tayari muda wote kumpa msaada wa malezi.
“Hivyo
unasema unataka watoto 2? Hapana, ningependa upate watoto 5 kama ulivyosema
awali. Najua ni shinikizo kubwa kulea watoto 5 lakini ningependa kukuhakikishia
kwamba wakati utakuwa unahisi ni mzigo mzito, wewe walete tu kwangu. Mimi nitakuwa
nyanya yao na nitawalea,” Diana Marua alimshauri
bintiye.
Mwisho wa siku, binti huyo alishawishika na ushauri
wa mamake kuhusu kupata watoto 5 lakini kwa sharti moja.
“Ndio
nitapata watoto 5 lakini kama hawatakuwa wasumbufu. Kama hawatakuwa wananiita
ita kila mara wakiniomba hiki na kile. Mwingine anasema sitaki kipakatalishi,
nataka simu,” Heaven Bahati alisema.
Diana alimwambia kuwa hivyo anavyosema hataki kuja
kusumbuliwa na wanawe ndivyo wanavyomsumbua, shtaka ambalo bintiye alijitetea
kwamba yeye si msumbufu vile.
Diana hata hivyo alimhakikishia kwamba hawamsumbui
bali ni furaha yake kuona uzao wat umbo lake wakimuitisha hiki na kile.
Diana Marua ni mama kwa watoto 5, watatu wakiwa wale
aliowazaa, mmoja akiwa wa kuasiliwa na mwingine akiwa ni wa mumewe na mpenzi
wake wa ujanani, Yvette Obura.