logo

NOW ON AIR

Listen in Live

P Diddy anawapigia simu mashahidi akiwa gerezani - waendesha mashtaka

Sean "Diddy" Combs amekuwa akivunja sheria za gereza kwa kuwasiliana na mashahidi .

image
na BBC NEWS

Burudani19 November 2024 - 12:42

Muhtasari


  • Nguli huyo wa muziki anashutumiwa kwa kufanya "juhudi nyingi" za "kushawishi mashahidi," kwa kutumia simu za wafungwa wengine.

Sean "Diddy" Combs amekuwa akivunja sheria za gereza kwa kuwasiliana na mashahidi katika kesi yake itakayo sikilizwa mahakamani juu ya utumwa wa ngono, wamedai waendesha mashtaka.

Nguli huyo wa muziki anashutumiwa kwa kufanya "juhudi nyingi" za "kushawishi mashahidi," kwa kutumia simu za wafungwa wengine, na kutumia mikutano ya kuzungumza kwa simu na watu ambao hawako kwenye orodha yake ya mawasiliano iliyoidhinishwa.

Waendesha mashitaka walisema pia katika jalada la mahakama kuwa, uhakiki wa simu zilizorekodiwa pia uligundua kuwa Combs aliagiza familia yake kuwasiliana na mashahidi watarajiwa katika kesi yake.

Miongoni mwa juhudi hizo, walinukuu ujumbe wa Instagram uliotumwa na mwanamke, anayepinga madai yaliyotolewa na mwimbaji Dawn Richard katika kesi dhidi ya Combs.

Waendesha mashitaka wanadai taarifa ya mwanamke huyo iliandaliwa na Combs wakati wa mawasiliano kwa ujumbe mfupi na simu nyingi kutokea gerezani.

Pia wanadai kulikuwa na mwelekeo wa wazi kwamba Combs alimlipa mwanamke huyo, baada ya kuchapisha ujumbe wake.

Combs, 55, kwa sasa yuko kizuizini huko Manhattan. Amekana mashtaka yote dhidi yake na amekanusha kufanya makosa yoyote.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved