Mwimbaji na mtunzi wa nyimbo kutoka Nigeria Peter Okoye,
maarufu kama Mr P ameonyesha ukomavu wake kiakili kwa kuweka uadui na ugomvi
wake na kakake kando wakati anasherehekea siku yao ya kuzaliwa.
Mr P alichukua kwenye kurasa zake kwenye mitandao ya kijamii
na kuchapisha picha zao za utotoni na wakiwa watu wazima na kufuatisha na
ujumbe wa kusherehekea siku ya kuzaliwa na pacha wake, Paul Okoye maarufu kama Rudeboy.
Hii ni licha ya Rudeboy kumburuza hadi kwa kutumia wakili
akidai kwamba pcha wake aliiba wimbo wake na kuutoa bila ridhaa yake.
Awali, Radiojambo.co.ke iliripoti kuwa Paul Okoye, almaarufu
Rude Boy, alimshutumu Bw P na mtayarishaji wao wa zamani, Vampire, kwa kuiba
nyimbo zake.
Alifichua kuwa alikuwa ameandika na kurekodi wimbo unaoitwa
‘Winning,’ ulionuiwa kuwa sehemu ya albamu yake ijayo mwaka ujao.
Hata hivyo, alidai kwa
mshangao kwamba Mr. P alitoa wimbo huo kupitia kwa mtayarishaji huyo.
Akijibu madai hayo, Mr. P alieleza kuwa wimbo huo aliutunga
yeye na Calypso60. Alidai kuwa haiwezekani kwake kuiba wimbo alioshirikiana
nao, kama alivyodai pacha wake.
Licha ya madai hayo yanayoendelea, Peter bado alikiri na
kumsherehekea kaka yake katika siku yao maalum. Alitumia ukurasa wake wa Instagram
kushiriki picha zao nzuri za kujirusha.
Aliandika picha hizo, “HAPPY BIRTHDAY TO US! Endelea
KUSHINDA! 🎂🎂🎂🙅🏽♂️🙅🏽♂️🎂🎂🎂#WinningSeaon
+1.”
Mapacha hao wawili kutoka kwa bendi iliyosambaratika ya
PSquare wamekuwa katika hali ya mfarakano kwa miezi kadhaa sasa.
Ugomvi wao ulianza mnamo mwaka 2015 lakini baada ya miaka
kadhaa walitangaza kusameheana na kurudiana mwaka 2021
Baada ya uvumi wa kuachana, wawili hao walionyesha hadharani
ufa mkubwa katika undugu wao mwaka 2017 walipofarakana hadharani kupelekea
kusitisha shoo zao walizokuwa wameziratibu kufanyika Marekani na Kanada wakati
huo.
Baada ya kurekebisha uhusiano wao 2021, waliingia studio na
kuachia wimbo kwa jina ‘Jaiye’ ambao hata hivyo ulifanikiwa kuwaweka pamoja kwa
kipindi kifupi.
Walikorofishana tena mwaka jana ambapo wamekuwa
wakituhumiana kwa sakata mbalimbali ambazo ziliangusha PSquare.