Mwanasosholaiti Vera Sidika amewonyesha picha ya
pamoja na wanawe waliokua na kufichua kwamba hakuna kitu chenye thamani zaidi
katika maisha yake zaidi ya wanawe.
Mama huyo wa watroto wawili, Asia na Ice Brown
alionyesha picha akiwa amefananisha mavazi na wanawe na kusema kwamba hajutii
hata kidogo kuwa mama kwa malaika hao wawili.
Vera Sidika alisema kwamba kuwa mama ni hisia moja ya
kipekee ambayo humpa mwanamke uwezo wa kugundua kuwa ana kipaji kingine cha
nguvu za kipekee ambazo asingejua kuwa anazo kabla ya kuwa mama.
“Furaha
yangu kuu; watoto wangu 😍🥹❤️ Kuwa mama ni kujifunza
kuhusu nguvu ambazo hukujua kuwa nazo, na kukabiliana na woga ambao hukujua,”
Vera Sidika aliandika.
Hii ni mara nyingine Sidika anaudhihirishia ulimwengu
kuwa yeye ni mama bora kwa wanawe, kwani aghalabu huonekana akiwa mbioni
kusafiri katika mataifa mbalimbali jambo linalozua maswali kuhusu muda wa kukaa
karibu na wanawe.
Safari zake za mara kwa mara kwa kutumia ndege
akizuru mataifa mbalimbali zimefanya baadhi kuibua maswali kuhusu Chanzo cha
pesa zake, jambo ambalo Sidika alijibu kwamba yeye huvuna kutokana na
kujivinjari tu.
Wakati wa kipindi cha Maswali na Majibu na wafuasi wake wa
Instagram mnamo Ijumaa usiku Desemba 6, 2024, shabiki mmoja aliuliza sosholaiti
swali hilo akilini mwa kila mtu:
“Unafanya kazi gani?”
Katika mtindo wake wa kawaida wa kujibu, Vera alijibu,
"Mimi ni mtu wa kutulia sana," na kumwacha shabiki, na wengine wengi,
bila maelezo ya kina ya jinsi anavyopata riziki yake.
Tangu kujipatia umaarufu kupitia kuonekana kwake katika
tasnia ya burudani nchini Kenya, zikiwemo video za muziki na vipindi vya hali
halisi kwenye televisheni, Vera ametambulika kote kwa utu wake wa ujasiri,
mtindo wa kipekee wa mitindo na maisha ya kifahari.
Sosholaiti huyo ametumia vyema umaarufu wake, akibadilisha
njia za mapato yake ili kujenga chapa inayodumisha maisha yake ya hali ya juu.
Vera Sidika amewekeza katika tasnia ya urembo, akimiliki
chumba cha urembo na spa ambacho hutoa huduma kama vile matibabu ya ngozi,
utunzaji wa nywele na uboreshaji mwingine wa urembo.