Kampuni ya Google, mnamo Jumanne asubuhi, ilitoa orodha za vitu na watu waliofuatiliwa zaidi nchini Kenya mwaka wa 2024.
Orodha hiyo ilijumuisha watu, vitu na mada ambazo zilitafutwa sana kuanzia mwezi Januari hadi Desemba mwaka huu.
Kulingana na Google, SHA, Gachagua, Vybz Kartel, Brian Chira, AFCON, Supacell, na Anguka Nayo yanaongoza kwenye vitu vilivyofuatiliwa zaidi nchini Kenya.
Maneno ya nyimbo za Kudade, Hit and Run ya Sheensea, Set it, Mimi ni Mzabibu Baba Ni Mkulima na Not Like Us pia yalitafutwa sana kwenye Google.
Nyimbo zingine ambazo zilitafutwa sana ni pamoja na nyimbo za Not like Us, Viviano, Nina Siri Naye Yesu, Ameniweka Huru Kweli, na Maombi Yangu Yafike Kwako.
Watu wa kimataifa ambao walisakwa zaidi nchini Kenya mwaka wa; Vybz Kartel, Donald Trump, Benny Hinn, Kamala Harris, Baltasar Engonga, Joe Biden, Diddy, Bonny Mwaitage, King Charles na Katt Williams.
Wakenya walitafutwa zaidi kwenye Google nchini mwaka wa 2024 ni;
1. Gachagua (Naibu rais wa zamani)
2. Rebecca Miano (Waziri wa Utalii)
3. Soipan Tuya (Waziri wa Ulinzi)
4. Noordin Haji (Bosi wa NIS
5. Kindiki (Naibu Rais)
6. Robert Nagila (Mwanahabari)
7. Kawira Mwangaza (Gavana wa Meru)
8. Jimmy Wanjigi (Mwanasiasa, Mfanyibiashara)
9. John Mbadi (Waziri wa Fedha)
10. Mutuse (Mbunge, Kibwezi Magharibi)
Vifo vilivyofuatiliwa zaidi kwenye Google nchini Kenya 2024
ni;
1. Brian
Chira - Mtayarishaji Maudhui (Machi 16)
2. Charles
Ouda - Muigizaji (Feb 3)
3. Rita
Tinina – Mwanahabari (Machi 17)
4. Kelvin
Kiptum – Mwanariadha (Feb 11)
5. Fred
Omondi – Mchekeshaji (Juni 15)
6. Allan
Kiuna – Askofu (Julai 9)
7. Mr Ibu –
Muigizaji (Machi 2)
8. Njambi
Koikai – Mtangazaji (Juni 3)
9. Lizzie
Wanyoike – Mjasiriamali (Jan 14)
10. PeetahMorgan
– Mwimbaji (Feb 25)