Cross-dresser maarufu
kutoka Nigeria, Idris Okuneye maarufu kama Bobrisky amezua mjadala pevui
mitandaoni baada ya kuweka wazi malalamiko anayopitia kama mwanamke.
Bobrisky, mwanamume
aliyebadili jinsia yake na kuwa mwanamke kupitia msururu wa upasuaji mbalimbali
alipeleka kwenye Instagram akilalamika kwa hedhi yake huwa na uchungu mno.
Akionekana kulalamikia
maisha magumu na ya uchungu tele wanayopitia wanawake, Bobrisky alifichua
kwamba wakati mwingine yeye hulia anapoona hedhi yake, akisema kuwa ni ya
uchungu mkali.
“Kusema kweli sasa hivi
najihisi kabisa kuwa mwanamke aliyekamilika. Wakati mwingine huwa navunjika kwa
kilio wakati niko kwenye siku zangu za mwezi, kwa sababu ni uchungu sana,”
Bobrisky aliandika.
Watumizi wa Instagram walifurika
kwenye chapisho hilo wakimsuta vikali wengine wakihisi anawatania kuhusu siku
za mwezi kwani yeye bado ni wa jinsia ya kiume hata kama anajitambua kama
mwanamke kupitia upasuaji.
Haya hapa baadhi ya
maoni;
Anthony Omoni alisema,
"Wanaume walichukua mada ya mwaka "No gree for anybody. Mama wa Lagos
ni mwanamume, mwanamke aliyevaa vizuri ni Mwanaume, binti wa kifalme wa Afrika
ni mwanamume, Tinubu anafaa kumteua Mwanaume kama Waziri. wa Masuala ya
Wanawake”.
Rietta aliuliza,
"Hedhi ni kumwaga kitani cha tumbo kwa hivyo nimechanganyikiwa, je,
wanaume pia wana tumbo?".
Muhammed Baaheer
alibainisha, "Nasubiri kusikia ujauzito mwezi ujao kipindi hicho ambacho
hutaona siku zako za mwezi".