RAPA na YouTuber Diana
Marua ni mmoja kati ya washawishi wa mitandao ya kijamii wa humu nchini ambao
wanamaliza mwaka wa 2024 kwa furaha na ari ya ajabu.
Mama huyo wa watoto
watatu amefichua kwa mashabiki wake kwamba yeye hatokuwa miongoni mwa wale
wanaomaliza mwaka kwa kinyonge, kwani umekuwa moja kati ya miaka yenye
mafanikio ya kipekee katika maisha yake.
Zikiwa zimesalia siku 20
tu kukunja jamvi la 2024, Diana Marua ameweka wazi kwamba anamaliza mwaka kwa
nguvu kwani tayari ameshajikusanyia vipande 8 vya mashamba katika Maeneo mbalimbali
nchini kwa mwaka huu pekee.
Alipiga picha akiwa na
hatimiliki 8 za mashamba yake, akisema kwamba lengo ni kuendelea kuongeza
utajiri wake mwaka ujao, kwani hii ni mwanzo tu.
“Lengo ni kumaliza imara
💪🏻
mwaka gani! 2024, hatimiliki 8 tajiri zaidi 🥹 🙏
Nimetimiza ndoto yangu ya 2024! 🙌 Hatimaye nilipata vipande vya ardhi
katika maeneo tofauti, na hebu niambie - hiyo kitu imenitoka!”
Diana Marua aliandika kwa furaha ya ajabu.
Mke huyo wa msanii
Bahati Kioko bila shaka ni mmoja wa wale ambao bidii yao imedhihiri wazi wazi
kwa matokeo mwaka huu.
Huu ndio mwaka ambao
Diana Marua na mpenziwe Bahati Kioko walikuwa wanandoa wa kwanza kufanikisha
shoo yao ya kihalisia katika jukwaa kubwa la utiririshaji la Netflix.
Marua na Bahati pia
waliweza kumtambulisha mtandaoni binti yao, Malaika ambaye hivi majuzi
amesherehekea kutimiza umri wa miaka miwili.