Wakili wa rapa Jay-Z ameiomba mahakama itupilie mbali kesi inayomhusisha mteja wake na nguliwa wa muziki Sean "Diddy" Combs kwa kumbaka msichana wa miaka 13 mwaka 2000, baada ya kuibuka kwa hoja za kutofautiana katika tuhuma dhihi yake.
Mwanamke wa Alabama, aliyetajwa katika hatua ya kisheria na jina bandia Jane Doe, amewashutumu wanamuziki hao kwa kumwekea dawa za kulevya na kumshambulia kwenye sherehe ya nyumbani kufuatia Tuzo za Muziki za Video za MTV.
Alidai alizungumza na mtu mashuhuri kwenye sherehe, japo mwakilishi wake alisema alikuwa kwenye ziara wakati huo.
Baba yake aliambia NBC News kuwa hakumbuki akiendesha gari kwa saa tano kumchukua baada ya madai ya kushambuliwa, kama asemavyo.
Katika mahojiano na NBC, mwanamke huyo alikiri kufanya "makosa" katika mashtaka yake, lakini akasema hajabadili msimamo kuhusu madai yake.
Wahudumu wanaotoa usaidizi kwa waathiriwa wa ubakaji wanasema ni jambo la kawaida kwa waathiriwa wa mashambulio kama hayo kukumbuka baadhi ya maelezo, haswa ikiwa wametiliwa dawa za kulevya.