
Willard Carroll Smith II maarufu kama Will Smith amekana madai yanayomhusisha na msaani wa rap P-Diddy ambaye alikamatwa na kushtakiwa kwa tuhuma ya kujihusisha katika ulanguzi wa binadamu na hatia nyinginezo.
Mwanafilamu na mwimbaji huyo wa nyimbo za rap maarufu kama Will Smith mwishowe alifunguka na kuzungumza kuhusu tuhuma kuwa alijihusisha katika sherehe za rafiki yake P-Diddy, sherehe iliyobahatizwa kama Freak off Party ambapo inadaiwa kuwa hatia kadhaa za kingono zilifanyika.
Nyota huyo wa filamu ambaye alizaliwa 25 Septemba 1998 alikanusha uvumi huo kuwa hauna msingi. Akiongea katika tamasha moja eneo la Sandiego, Califonia, Smith alisema kuwa uvumi huo ni mbaya na unafaa kukoma.
‘’Nimekuwa nikiona utani na kila kitu, nyingine zinafurahisha na nyingine zinahuzunisha. Nataka kuweka hili wazi kabisa: Sina chochote cha kufanya na Puffy, kwa hivyo unaweza kuacha huo utani . Na mkome huo upuuzi. Sijafika popote karibu na "Freak Off." Alisema Smith.
Nyota huyo wa kuigiza aliendelea kukanusha kuwa hajawaifanya hayo mambo aliyoyaita ya kijinga wala hapendi mafuta ya watoto. Maoni haya yanakuja baada ya chupa kadhaa za mafuta za watoto kupatikana katika mojawapo ya makao ya P-Diddy wakati maafisawauchunguzi wa biashara ya ngono kuvamia jumba lake.
Smith alimaliza kwa kusema kuwa anafanya vitu vyake kibinafsi na hahitaji kuhusishwa na vitu vya watu wengine.
P-Diddy bado yuko korokoroni anakozuiliwa Brooklyn, New York huku akichunguzwa kwa madai ya kesi kadhaa ikiwemo unyanyasaji wa kijinsia, biashara ya ngono, ulaghai na kuwezesha ukahaba.