CHUO kikuu cha Kisii
kimeonesha fahari yake katika uendelevu baada ya kuongeza msafara wa magari
mengine mapya katika orodha ya magari yanayomilikiwa na chuo hicho.
Kupitia ukurasa wao wa
Facebook, Chuo hicho kilitaarifu umma kwamba wamefanikiwa kununua ambulensi
mpya ya kisasa kwa ajili ya kuwahudumia jamii ya chuo hicho.
Kando na ambulensi, chuo
hicho pia kilionesha picha za mabasi mawili mapya yenye uwezo wa kubeba abiria
67 kila moja.
“Kwa furaha, shauku na
furaha isiyoisha, familia ya Chuo Kikuu cha Kisii leo imekaribisha Ambulansi ya
kisasa, ya kitaalamu na iliyo na vifaa vya kutosha pamoja na mabasi mawili ya
kubeba watu 67 kila moja,” uongozi wa chuo
ulisema.
Wakitetea hatua hiyo,
chuo hicho kilisema kwamba hii ni moja ya mkakati wa kuboresha huduma kwa jamii
nzima ya chuo hicho.
“Nyongeza 3 ni uamuzi wa kimkakati unaokaribishwa
sana na Baraza la Chuo Kikuu na utasaidia sana katika kuhakikisha utendakazi
katika Chuo Kikuu unakuwa bora zaidi,” waliongeza.
Wakati akiwaalika,
Mwenyekiti wa Baraza alifurahishwa na maendeleo ya ajabu ya Chuo Kikuu cha
Kisii.
Chuo kikuu cha Kisii ni
miuongoni mwa vyuo vichache ambavyo vinaonyesha maendeleo makubwa wakati ambapo
idadi kubwa ya vyuo vikuu vya serikali vinapitia changamoto za kifedha.
Vyuo vikuu kama Moi na
Nairobi vimekuwa katika wakati mgumu miaka ya hivi karibuni kutokana na kile
kinachokisiwa kuwa ni kutokuwa na hela za kutosha kuendeleza shuli vyuoni humo.