MSANII wa muziki wa Nigeria, Tiwa Savage amefunguka
kuhusu talaka yake na aliyekuwa mpenzi wake Tunji ‘TeeBillz’ Balogun, na
kufichua changamoto alizokumbana nazo wakati na baada ya kutengana kwao mwaka
wa 2018.
Akiongea kwenye The Receipts Podcast, mwimbaji huyo
alifichua kwamba mume wake wa zamani ndiye aliyehusika na mgawanyiko wao, ambao
ulitokea wakati wa mapambano yake na unyogovu wa baada ya kujifungua.
Msichana huyo mwenye umri wa miaka 44 alielezea
shutuma kali alizovumilia, huku Wanigeria wengi wakimgeuka na kushambulia tabia
yake.
Alikumbuka jinsi watu mashuhuri walivyomshauri anyamaze
ili kuhifadhi sifa yake, hata hali hiyo ilipozidi kumsumbua kihisia.
Tiwa alisimulia jinsi TeeBillz alitangaza maswala yao
ya ndoa mtandaoni, na kumwacha kubeba mzigo wa chuki za umma.
"Nilipotoka,
nilikuwa mpenzi wa Nigeria nilipoanza na sikuweza kufanya kosa lolote machoni
pa Mnigeria. Nilifanya kila kitu kama ilivyotakikana. Nilienda chuo kikuu na
sikuwa mama mtoto. Niliolewa kisha nikapata mtoto kwa hivyo nilifanya kila kitu
kwa mpangilio sahihi na kila mtu alinipenda kisha kila kitu kilifanyika.”
“Kisha
nikaanza kupata chuki kutoka kwenye blogu na nikaanza kupata chuki kutoka kwa
watu fulani. Jinsi hali yetu ilivyotokea, alitangaza mtandaoni. Sikuachana naye
lakini mimi ndiye nilikuwa nashambuliwa.”
Baada ya kujaribu kushiriki upande wake wa hadithi,
mwimbaji alisema ukosoaji ulizidi.
“Watu
walisema, ‘Unathubutu vipi kwenda kuzungumza?’ Niliambiwa singeshinda kamwe kwa
sababu nilikuwa mwanamke. Ilikuwa ya kuhuzunisha moyo.”
"Wakati huo, mtoto wangu alikuwa na umri wa
miezi michache tu na nilikuwa nikiugua baada ya kujifungua na mwili wangu
haukuwa sawa na nilikuwa na huzuni. Kisha kila mtu alikwenda kwake na watu
wachache tu walikuja kuniona.”
“Baada
ya kuhojiwa ili kueleza upande wangu, hali ilizidi kuwa mbaya. Watu walikuwa
kama ‘Unathubutu vipi kwenda kuzungumza’ ‘Wewe ni mwanamke na unatakiwa kujenga
nyumba, ni kosa lako’.”
"Nakumbuka
watu mashuhuri walinipigia simu kuniuliza jinsi ningeweza kusema upande wangu
wa hadithi kwa sababu singeshinda kamwe. Tangu wakati huo, nilikuwa kama
sitawahi kuzungumzia hali hiyo kwa sababu ilihuzunisha sana jinsi umma
ulivyoichukulia na kunilaumu.”
"Ilinifungua
macho na ilinifanya nishuke moyo kwa muda mrefu. Ilinikasirisha kisha nikawa
‘Msichana Mbaya wa Kiafrika.’
“Nilijiwazia
kuwa baada ya kufanya kila kitu sawa bado nilishambuliwa. Kisha nikaanza
kuchora tattoo na kuvaa sketi fupi na bikini. Nilikuwa mshamba tu,” Alisimulia
mama huyo wa mtoto mmoja.