BIEN, msanii kiongozi wa iliyokuwa bendi ya Sauti Sol
kwa mara ya kwanza amefunguka kuhusu kutokuwa na watoto katika ndoa yake na
mkewe, Chiki Kuruka.
Akizungumza na Mungai Eve wakati wa maandalizi ya
jukwaa la tamasha la Sol Fest katyika uwanja wa Uhuru Gardens, Bien alisema
kwamba hata yeye angependa kuwa na watoto lakini suala hilo si la kukurupukia.
Msanii huyo ambaye amepata mafanikio makubwa kimuziki
haswa mwaka huu kwa kufanya ngoma nyingi zilizowavutia mashabiki wake, alisema
kwamba wengi wanaona hana mtoto katika ndoa yake na kuanza kumhukumu bila kujua
kwamba ni suala ambalo hata yeye analiratibu kwa muda wake.
Alikanusha uvumi kwamba hataki kuwa na watoto katika
maisha yake, akiwasihi mashabiki wake kumuombea yeye na mkewe kwani suala la
kutafuta mtoto litafanyika hivi karibuni.
“Mimi
nitakuwa na watoto, watu tulieni. Lakini ni vile nilihitaji kuwa tayari. Mimi nafanya
vitu na mwendo wangu na mwendo wa Mungu.”
“Nafikiri
kuwa katika uhusiano wa ndoa inayofanya kazi imepekea ndoa yetu katika kiwango
kingine, kiasi kwamba tumependana sasa ile kwamba tukizaa mtoto anaingia katika
tassisi iliyojawa mapenzi ya ajabu. Na si eti awali hatukuwa tunapendana,
lakini sasa hivi jinsi tunafanya kazi pamoja huu ndio wakati muhimu wa kuwa na
watoto, hivyo tuko katika hiyo safari na watu mtuombee,”
Bien alisema.
Akizungumza kuhusu siri ya kudumu kwa ndoa yake
katika wakati ambapo watu wengi maarufu ndoa zao zinavunjika, Bien alisema kuwa
siri ni kuweka uhusiano wake mbali na mitandao ya kijamii.
“Chenye
mimi hujaribu kadri ya uwezo wangu ni kutoweka mapenzi yangu mtandaoni. Mimi na
mke wangu tunapendana na tunajua tunapendana. Hivyo tutapostiana ndio
mitandaoni lakini haikuwi eti ndicho kitu main kwenye ukurasa wangu eti
kuonyesha mapenzi. Kwa sababu hiki ndicho kitu cha pekee ambacho ninakipenda,
hivyo lazima nikilinde,” Bien alifunguka.