MCHUMBA
wa zamani wa Enzo Fernandez amefichua jinsi nyota huyo wa Chelsea alivyomaliza
uhusiano wao ghafla licha ya kuwa na watoto wawili pamoja.
Fernandez alikuwa na Valentina Cervantes tangu
walipokuwa vijana, wakati kiungo huyo alipokuwa akiichezea River Plate ya
Argentina, kabla ya kupata ujauzito akiwa na umri wa miaka 19 na baadaye
kuhamia Benfica na Chelsea.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 aliigharimu
Chelsea pauni milioni 107 baada ya kusajiliwa mwaka 2023 kufuatia ushindi wake
wa Kombe la Dunia akiwa na Argentina.
Wawili hao walihamia katika nyumba moja huko London
pamoja na binti yao Olivia na mwana wao Benjamin, wakiishi huko kwa karibu
miaka miwili kabla ya Fernandez kuwasilisha habari za mshtuko kwa mpenzi wake
mnamo Oktoba.
Akiongea na Game, Set & Match, Cervantes alisema:
"Kila kitu kilikuwa sawa na ghafla siku moja aliniambia kuwa hataki kuwa
[na mimi] tena. Kuna mambo ambayo bado natakiwa kuyashughulikia, lakini ndivyo
hivyo, niliikubali."
Alisema alilia kwa dakika tano baada ya kuvunja
habari hiyo na kuongeza kuwa alikataa ombi lake la kumruhusu yeye na watoto
kubaki naye nyumbani - na kuishia kuhamia Argentina.
"Enzo
alinipa nafasi ya kukaa kwenye nyumba ile ile tuliyokuwa tunaishi na kuniambia
kuwa anaenda kupanga sehemu nyingine, lakini nilimwambia nitarudi Argentina kwa
ajili ya familia yangu. Kwa sababu nilitoa kila kitu katika uhusiano huo na
sijui, sijutii chochote, lakini kila kitu nilichofanya ni kwa ajili yake na kwa
ajili ya familia tuliyounda."
Cervantes pia alizungumzia jinsi alivyotumia mshahara
wake wote kwa Fernandez wakati wa siku za mwanzo za maisha yake ya soka
alipokuwa akifanyia kazi mgahawa na kusomea shahada ya sheria.
Alisema: "Wakati huo nilipata zaidi ya [klabu]
ilimpa, tulitumia mshahara wangu wote, sikuwa na chochote cha ku’save."
Alipoulizwa kama bado anampenda Fernandez, aliongeza:
"Nafikiri
upendo bado upo kwa sababu ni vigumu sana kuondoka haraka. Sitegemei mwanaume
au mtu yeyote kuwa na furaha. Nikiwa na watoto wangu. Nitakuwa na furaha
daima."
Katika mahojiano mengine na Minuto Uno, aliendelea:
"Kila mtu anaichukua na kupitia michakato tofauti, nilijaribu kwenda
upande wa afya. Nampenda Enzo, siwezi kumdharau. Ni mtu ambaye aliandamana nami
kwa miaka mingi. nami pia nilifuatana naye, na nitaendelea kuandamana
naye."