WAZIRI wa zamani wa jinsia, utamaduni, sanaa na
torati za taifa, Aisha Jumwa alizua vichekesho Ijumaa wakati alihudhuria hafla
ya seneta wa kaunti ya Tana River, Danson Mungatana.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi kadhaa akiwemo
naibu wa rais Kithure Kindiki na waziri wa madini na uchumi wa baharini Ali
Hassan Joho.
Viuongozi wengi waliosimama na kuzungumza walisimulia
jinsi walikuja kujuana na Mungatana na ilipofika zamu ya Jumwa, aliwachekesha
wengi alipotania kwamba hajui mbona Mungatana hakumuona wakati wakiwa wadogo
licha ya urembo wake.
Jumwa alitania kwamba akiwa binti mdogo alikuwa
mrembo sana, akisema kwamba sasa hivi kidogo urembo umepunguka, na kuhoji kwa
nini Mungatana hakuona urembo wake uliopitiliza na pengine kumuoa.
“Mimi
ninafanana na babangu sana, na wakati huo babangu alikuwa ni mtu wa mambo mambo
kiasi, hivyo wakili wake akawa ni mheshimiwa Mungatana. Mimi nilimjua Mungatana
kama wakili wa babangu nikiwa msichana mdogo mrembo, si sasa hivi mambo
yameisha lakini sijui kwa nini Mungatana hakuniona wakati huo,”
Aisha Jumwa alitania huku watu wakijiachilia kwa vicheko.
Hata hivyo, waziri huyo wa zamani alishukuru jinsi
hatima ilikuja kufanya maisha yao baadae, akifichua kwamba sasa hivi Mungatana
ni shemeji yake.
“Lakini
hata hivyo nashukuru kwa sababu Mungatana sasa ni shemeji yangu nan iko na raha
sana,” Jumwa alimaliza utani wake.
Seneta Mungatana aliandaa hafla hiyo ya shukrani na
kurudi nyumbani kwake katika kijiji chake cha Ngao kaunti ya Tana River, hafla
ambayo iliwavutia hadi spika wa seneti, Amason Kingi.