TIKTOKER Rachael Otuoma ameonyesha kuvunjika moyo
vipande vuipande baada ya mumewe Ezekiel Otuoma kufariki dunia.
Rachael alithibitisha taarifa hizi kupitia ukurasa
wake wa TikTok ambayo alifichua kwamba Otuoma alifariki wakati Rachael
aqkifanya maandalizi ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kufanyika.
Rachael ambaye amekuwa wa msaada mkubwa kwa Otuoma
tangu 2020 alipopatikana na ugonjwa wa kufifisha neva mwilini, alitaja kifo cha
mpenzi wake kama pigo lisiloweza sahaulika.
“Kwa
Mume wangu😭💔Umeacha
shimo moyoni mwangu ambalo hakuna mtu mwingine awezaye kulijaza Japo ilikuwa
hivi karibuni sana💔thats
really broke my heart 😭
uliondoka kwenye birthday yangu 💔haitakuwa sawa tena nilikupenda sana
katika kifo nakupenda bado moyoni mwangu unashikilia nafasi ambayo wewe pekee
unaweza kuijaza😭😭😭Ilinivunja
moyo wangu kukufungua lakini hukuenda peke yako, umeenda na sehemu yangu pia😭😭😭💔💔💔💔💔MPAKA
MIMI TUKUTANE TENA,” Rachael aliandika kwa kuomboleza.
Ezekiel Otuoma amepumzika baada ya vita vya muda
mrefu na Motor Neuron Disease. Motor neurone ugonjwa ni hali ambayo huathiri
neva, husababisha udhaifu katika misuli, na kusababisha hatimaye kupooza.
Aligunduliwa na ugonjwa huo mnamo 2020.
Otuoma alichezea Ushuru Fc,Fc Talanta, AFC Leopards, Western Stima, Ulinzi Stars na Muhoroni Youth kabla ya kuachana na soka kutokana na hali yake ya kiafya.