Filamu ambayo inatarajiwa kuweka wazi baadhi ya madhambi
ambayo msaani na mwanafilamu tajika P-diddy aliyafanya sasa inasubiriwa kwa
hamu na ghamu ikitarajiwa kuonyeshwa kwa mara ya kwanza kupitia Peacock.
Kionjo cha ‘’The Making of a Bad Boy’’ imefichua kuwa watu wa karibu wa Combs, akiwemo mlinzi wake wa zamani, mfanyakazi wa ndani, msanii wa kupodoa na mtayarishaji ni miongoni mwa wanaohojiwa kwenye filamu hiyo.
Mwimbaji na mtayarishaji wa nyimbo na filamu Al B, atazungumza kwa mara ya kwanza kuhusu uhusiano wake na Kim Porter kabla hajachumbiana na Combs
Itakumbukwa kuwa Combs pia amekabiliwa na mashtaka zaidi ya 25 ya madai yake ya utovu wa maadili ya ngono miongoni mwa madai mengine.
Msaani huyo mwenye umri wa miaka 55 anazuiliwa katika gereza la Metropolitan Detention Center huko Brooklyn, New York, tangu Septemba, alipokamatwa kwa makosa ya biashara ya ngono na ulaghai. Majaji watatu tofauti wamemnyima dhamana kwa nyakati tatu tofauti.
Mawakili wa Sean "Diddy" Combs hata hivyo walikosoa filamu hiyo katika taarifa waliotoa kupitia jarida la Newsweek siku ya Ijumaa.
"Filamu hizi ni pamoja na madai ambayo hayajadhibitiwa na hutoa majukwaa ya nadharia za njama zisizo na msingi bila uwajibikaji au ushahidi. Kwa upande wa filamu ya Peacock haswa, motisha na uaminifu wa wale wanaohojiwa lazima utiliwe shaka. Wengi hudai kuwa na ujuzi lakini hawana uhusiano wowote na ukweli, huku nadharia zao potovu, zisizo na msingi zikikatwa na kusisitizwa ili zionekane kuwa za kweli,’’ Hii ni mujibu ya mawakili hao kupitia jarida la Newsweek.
Kesi ya biashara ya ngono ya Combs inatarajiwa kuanza mjini New York Mei 5 mwaka huu wa 2025.