BINTI wa rais, Charlene Ruto ametangaza ujio wa shindano lake jipya kwa vijana ambalo litafanyika mwezi ujao.
Kupitia ukurasa wake wa
X, binti wa kwanza wa rais Ruto alifichua kwamba vijana wenye talanta katika
ubunifu wa mitandaoni wenye kati ya umri wa miaka 18 hadi 35 wanaweza
jiandikisha.
Alisema kwamba ili
kujisajili, vijana ni sharti wajiunge kwa makundi ya watu 3 na kuonyesha ueledi
wao katika suala la kubuni wavuni, kujisajili kutaendelea hadi Februari 11.
“Ni wakati wa jambo letu
kubwa linalofuata…. Mashindano ya Tovuti! Je, wewe ni kati ya miaka 18-35?
Ungana katika vikundi vya watu 3 na utuonyeshe ulichonacho! Changamoto
itafunguliwa: 11 Januari 2025. Makataa ya kuwasilisha: 11 Februari 2025, saa
sita usiku. Hatua za kuhitimu:
1 Shiriki viungo vya
tovuti 3 bora ambazo timu yako au wanachama wameunda.
2️⃣
Tutumie pendekezo fupi la kiufundi la tovuti ambayo ungeunda kwa ajili ya
TYPNI.
3️⃣
Ambatisha vitambulisho na wasifu wa washiriki wote 3 wa timu.
Shinda $1,500 USD! Wacha
tuone ubunifu wako unang'aa. Tayari? Hebu tufanye hivi!” Charlene
aliandika.
Hii si mara ya kwanza
kwa binti wa rais kutangaza shindano la kuwakimu vijana wenye ujuzi katika
ubunifu wa mtandaoni.
Mwaka jana, binti Ruto
alitangaza shindano sawia na hilo lililofanyika majira sawia, na tuzo kwa
mshindi ilikuwa shilingi laki moja taslimu.
Kando na taslimu,
Charlene Ruto wakati huo alitangaza kula chakula cha mchana na mshindi katika
mgahawa wa kifahari.
“Mtandao wa Vijana wa Kimataifa (TYPNI) unatafuta
nembo bainifu inayojumuisha ari ya ujana na ubunifu. Shindano hili linatoa
fursa kwa wabunifu wachanga kuonyesha vipaji vyao na kuchangia utambulisho
mahiri wa TYPNI,” aliandika kwenye bango hilo kwenye mtandao
wa X.