MUIGIZAJI Sandra Dacha amefichua kwamba safari yake ya kupunguza uzani wa mwili wake imekuwa ikizaa matunda chanya kwa miezi minne sasa.
Mrembo huyo mwenye unene
alisema kwamba aliamua kuingia katika safari ya kupunguza uzai baada ya
kushauriwa na daktari kwamba alikuwa amefika hatua ya mwisho kabisa katika
unene, ambayo si ishara nzuri kwa afya yake.
Hapo ndipo aliamua
kutafuta njia ya kupunguza uzani wake, na ana furaha kwamba miezi minne baadae,
amepunguza angalau hai kilo 17 na anafurahia maendeleo ya safari yake ya kukata
uzito.
“Nilihisi mgonjwa,
nikaenda hospitalini, nikapimwa na nikagundulika kuwa nina nimonia. Nesi
alinivuta pembeni akaniambia ni muhimu ikiwa nitapunguza uzito kwa sababu
nilikuwa nimezidi unene🤣i was now at "GREATER MORBID OBESITY"
Hizi ni hatua za mwisho za unono😂hapa ukipita sasa wewe tunakuwachia
tu Mungu.”
“Ili kufupisha hadithi
ndefu...niliamua kutafuta suluhu na ndipo nilipokutana na @dr_arshni_malde wa
@tiaclinicskenya na Kuanza safari yangu ya kupunguza uzito OZEMPIC Agosti mwaka
jana…huu ni mwezi wangu wa Nne na ninaupenda😇 Nilikuwa na uzito wa kilo 152 na
leo nina 135kgs. Kupunguza kilo 1 kwa wiki,” Dacha
alisema.
Licha ya ‘The Biggest
Machine’ kufurahia kupunguza uzani kutoka kilo 152 hadi 135, bado anahisi
safari yake ingali mbali kutoka kufika mwisho kwani analenga kupunguza hai
angalau 115kgs.
Alisema kwamba awali
kabla aache kuzingatia ongezeko la unene wa mwili wake, alikuwa anatembelea
uzani wa kati ya kilo 115 na 123.
Dacha alisema kwamba
alikuwa anataka kuweka kama siri safari yake ya kupnguza uzani lakini aligundua
baadhi ya watu wameshaanza kushuku kutokana na picha zake mtandaoni za hivi
karibuni.
“Nina safari ndefu.
Uvumilivu ni muhimu. Ninataka kurejea kilo zangu za kawaida…115,123 hapo. Nilitaka kushiriki
safari yangu ya kupunguza uzito baada ya mwaka mmoja lakini nimekuwa nikisoma
sehemu ya maoni wakati wowote ninapochapisha na ni wazi nyie walikuwa wameanza
kuniona nikipungua uzito hivyo nikasema kwanini nisiongee kuhusu hilo sasa🤷🏿♀️ ama niko na
kiherehere,” alimaliza kwa utani.