TIKTOKER Rachel Otuoma aliwapunga wengi kwa hotuba yake yenye ukakamavu wa kipekee wakati wa mazishi ya mume wake, mwanasoka Ezekiel Otuoma.
Mrembo huyo ambaye
aliganda na mumewe licha ya hali yake ya ugonjwa wa kupooza neva mwilini kwa
takribani miaka minne, alisema kwamba hana mpango wa kuasi kiapo chake cha
ndoa.
“Vile tulikutana
tukapendana, mapenzi hayakuwahi isha. Na mumeona vile nilikula kiapo cha kuwa
naye kwa hali mbaya na nzuri, hata mzee mwenyewe alisema ni kipo
itatutenganisha,” Rachael alianza.
“Hivyo, ilikuwa ni ‘for
better, for worse’ na sisi tulikuwa kwa hiyo ‘worse’ kwa miaka 4 tulikuwa
tunaingia mwaka wa 5,” Rachael aliongeza.
Alisema kwamba hali ya
ugonjwa wa Otuoma haikuwa rahisi lakini kadri muda ulivyozidi kusonga,
aliikubali hali hiyo, akisisitiza kwamba hatokuja kumsahau mwanasoka huyo
katika maisha yake.
Rachael alionyesha
waombolezaji pete yake ya ndoa na Otuoma na kufichua kwamba haitowahi kutoka
katika kidole chake katika maisha yake yote.
“Otuoma alipatikana na
ugonjwa wa Motor Neurone, na hiyo safari ya kushughulikia mgonjwa wa huo
ugonjwa sio rahisi. Inahitaji mtu ako na utu, kujitolea ama heshima yako kama
mwanamke.”
“Kwa kweli nili’heal na
hali ya Otuoma, kwa sababu huyu ni mtu nilipenda na bado nampenda nap eye yake
ndio hii nievaa, niko na pete mbili sasa. Haitawahi nitoka kwa mkono wangu,”
Rachel alisema huku akiwaonyesha waombolezaji pete hiyo kidoleni.
Akifunguka kwa nini
ameamua kuchukua uamuzi huo licha ya kutofanikiwa na mtoto na Otuoma, Rachel
alisema kwamba mwanasoka huyo alikuwa mtu mwenye mapenzi ya dhati kwake
aliyempa heshima yake kama mwanamke.
“Otuoma ataishi kwa moyo
wangu milele. Huyu mwanamke hapa (akiashiria kwenye jeneza) alinipenda kwa roho
yake yote, alinipa heshima kama mwanamke na kila kitu nilihitaji angenipa,”
alisema.
“Hata kitu chochote mama
yangu angetaka, huyu mwanamume angempa na hiyo ndio sababu nilimpa Otuoma
heshima inayomfaa,” aliongeza huku akifichua kwamba huu
ungekuwa maka wao wa 10 kwenye kumbukumbu ya ndoa.