SARAH Mtalii, afisa mkuu wa kampuni ya Bonfire Adventures amefichua kwamba kabla ya kutulia katika ndoa, aliwahi chumbiana na wanaume wenye taaluma nzuri tu.
Akizungumza na Dr Ofweneke, Sarah alisema kwamba
katika umri wake wa kati ya miaka 20-30, alichumbiana na wanaume wenye taaluma
nzuri lakini wote hawakumvutia kuolewa na hata mmoja wao.
“Katika
umri wangu wa 20-30, nilikuwa nimekutana na watu lakini sikuwahi vutiwa na
mmoja wao. Nilikuwa sasa natafuta mwanamume wa kunioa,”
alisema.
“Nilikuwa
natafuta mwanamume lakini sidhani walikuwa tayari kuwa wanaume. Sitaki kuwahukumu
lakini walikuwa ni watu wazuri. Pia mimi nilikuwa na chaguo langu katika
mwanamume. Nilikuwa natafuta mwanamume wa nguvu. Nafikiri nilichumbiana na
rubani, mtaalamu wa IT, mhandishi wa ujenzi wa nyumba… ni vile sitaki kuwataja
tu maana watu wanaweza wajua,” Sarah Kabu alisema.
Alieleza kwamba hata aliwahi chumbiana na mwanaume
mwenye utajiri wa kiwango cha bilionea lakini bado hakuvutiwa katika ndoa na
yeye.
Mama huyo alieleza kwamba licha ya kuchumbiana na
watu wa kipekee, aligundua kwamba watu wenye majina makubwa ingemkalia vigumu
kukaa nao na hapo ndipo aliamua kwamba roho yake inataka mtu wa kawaida tu.
“Nilichumbiana
na watu wa ajabu lakini niligundua hawa watu wa majina makubwa itanikalia
vigumu kuwa nao hivyo nikasema ninataka mtu wa kawaida. Nafikiri wakati
mwingine wale watu wenye majina makubwa pengine huwa wanataka tu kujibamba
lakini hawako tayari kuoa, na kwangu mimi nilikuwa natafuta mume. Na ndio maana
ilinikalia rahisi kuwaacha wote, hata mmoja wao alikuwa bilionea,”
Sarah alisema.
Sarah alifichua kwamba kabla hajaolewa, alikuwa
anawaogopa sana wanaume watanashati, japo alikiri kwamba baadhi ya ma’Ex wake
walikuwa watanashati wa ajabu.
‘Pengine
naweza sema kwamba kwa wakati huo kwa kweli nilikuwa nawaogopa sana wanaume
watanashati japo baadhi ya maEx wangu walikuwa watanashati kupindukia. Nilikuwa
nawaogopa sana kwa sababu unajua kila mwanamke anawataka,’
Sarah alifichua.