BREEDER LW, rapa wa Arbantone amewashangaza mashabiki wake baada ya kuelezea kiasi kikubwa zaidi cha hela ambazo aliwahi tumia kwa mwanamke.
Msanii huyo wa kibao maarufu ‘Dedi Dealilee’
alichapisha video kwenye Instagram yake akiwa katika kipindi cha kujibu maswali
na wenzake.
Kwenye maoni, shabiki wake mmoja alimtaka kujibu
kiasi cha juu zaidi cha pesa ambazo amewahi kutumia kumfurahisha mwanamke na
kwa mshangao, Breeder alifichua kwamba alitumia takribani laki 8.
“Kiasi
kikubwa cha pesa ushawahi tumia kwa mrembo?”
shabiki huyo alimuuliza.
“780K”
Breeder LW alijibu.
Baadhi ya watu walipigwa na butwaa wakihisi kwamba
kiasi hicho kwani si kawaida ya wanaume wengi wa Kenya – angalau kutokana na
utafiti wa awali.
Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali, Wanaume wa Kenya
hutumia pesa kununua vitu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na chakula, nyumba,
usafiri na vitu vya anasa. Wanaweza pia kutumia pesa katika kucheza kamari na
shughuli nyinginezo.
Sehemu kubwa ya mapato ya Mkenya huenda kwenye
chakula na vinywaji. Utafiti uligundua kuwa Wakenya hutumia kati ya Sh200 na
Sh399 kwa siku kununua chakula.
Wanaume matajiri wanaweza kutumia pesa kununua saa,
mikoba, viatu, manukato, na suti za bei ghali. Wanaume wengine wanaweza kutumia
pesa kununua pombe kwenye baa za kienyeji