logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mkenya ambaye amekuwa akifanya kazi katika Ikulu ya Marekani azungumza huku kazi yake ikiisha

Bi Irungu amezungumzia jinsi imekuwa heshima kufanya kazi kama mhariri wa picha wa makamu wa rais Kamala Harris.

image
na Samuel Mainajournalist

Burudani22 January 2025 - 09:24

Muhtasari


  • Mhariri huyo mahiri wa picha pia alizungumzia jinsi anavyojivunia kazi ambayo yeye na wenzake wamefanya katika ofisi ya picha ya Ikulu.
  • Bi Irungu amekuwa akifanya kazi kama mhariri wa picha wa Kamala Harris katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.


Bi Polly Irungu, mpiga picha wa Marekani mwenye asili ya Kenya ambaye amekuwa akifanya kazi katika afisi ya aliyekuwa makamu wa rais wa Marekani Kamala Harris ametoa shukrani zake huku utawala wa Biden-Harris ikifikia kikomo.

Donald Trump alichukua wadhifa wa rais wa Marekani mnamo Jumatatu, Januari 20, na kuhitimisha utawala wa Biden na Harris ambao waliondoka ofisini pamoja na wafanyikazi wao.

Huku akijiandaa kuondoka katika Ofisi ya Picha ya Ikulu ya Marekani ambako amekuwa akifanya kazi kwa zaidi ya miaka miwili iliyopita, Bi Irungu alizungumzia jinsi imekuwa heshima kufanya kazi kama mhariri wa picha wa makamu wa rais Kamala Harris.

"Imekuwa heshima kuona kupitia maelfu ya picha athari ambayo Makamu wa Rais Kamala Harris amekuwa nayo kwa nchi yetu. Kutumikia kama mhariri wa picha wa VP Harris kumekuwa jambo la kunyenyekeza na lenye kuthawabisha,” Bi Irungu alisema kupitia Instagram.

Mhariri huyo mahiri wa picha pia alizungumzia jinsi anavyojivunia kazi ambayo yeye na wenzake wamefanya katika ofisi ya picha ya Ikulu.

"Nina deni kubwa kwa Lawrence Jackson, Mkurugenzi wa Makamu wa Rais wa Upigaji picha, kwa kuniamini katika jukumu hili. Kama vile VP Kamala Harris anasema, "kazi ngumu ni kazi nzuri," na ninajivunia kazi nzuri ambayo tulifanya," alisema.

Bi Irungu amekuwa akifanya kazi kama mhariri wa picha wa makamu wa rais wa zamani wa Marekani Kamala Harris katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Mnamo Agosti mwaka jana, alisherehekea miaka miwili katika ofisi hiyo kuu nchini Marekani na akaeleza jinsi alivyofurahi kufanya kazi pale.

"Siwezi kuamini imekuwa miaka miwili katika Ofisi ya Picha ya Ikulu/Ofisi ya Makamu wa Rais. Ninashukuru sana kufanya kazi na kujifunza kutoka kwa walio bora zaidi, "alisema.

Kamala na Biden waliondoka ikulu ya Marekani tarehe 20 Januari ambapo walikikabidhi madaraka kwa Donald Trump ambaye alishinda uchaguzi wa urais mwaka jana.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved