Huku ulimwengu ukiendelea kuhamia
kidijitali, kampuni ya Radio Africa Group inajaribu kuleta mapinduzi katika
vyombo vya habari vya Kenya kwa kutambulisha jukwaa jipya la utiririshaji wa
kidijitali.
Programu ya Songa Play inaruhusu wasikilizaji kutiririsha vipindi vyao Radio Jambo wapendavyo, podikasti, mix za DJ na bidhaa zingine nzuri bila malipo.
Kwa muundo wake unachofaa mtumiaji, Songa Play inalenga kuvutia hadhira pana, ikitoa utiririshaji unaofikiwa, wa ubora wa juu.
Kwenye Songa Play, kuna sehemu y radio, mix za DJ, podikasti, nyumbani na wasifu wako.
Wakenya wanaweza kufikia vivutio vya vitengo wapendavyo vya Radio Jambo, kupata mix zote za stesheni moja kwa moja kwenye jukwaa, kusikiliza vipindi wavipendavyo moja kwa moja na kupiga gumzo na Radio Jambo moja kwa moja kwenye jukwaa.
Baadhi ya vipindi vya Radio Jambo vinavyopatikana kwenye programu ni Patanisho, Toboa Siri na Deadbeat.
Ili kufurahia vipindi hivi, ingia kwenye Songa Play kutumia kifaa chako, tafuta kwa urahisi kipindi ama kitengo utakacho, kisha ubofye kwenye ikoni inayoonyesha programu unayotaka ili kucheza.
Wakenya pia wanaweza kutiririsha vipindi vya moja kwa moja vya stesheni washirika wetu Classic 105, East FM, Gukena FM, Home Boyz radio, Kiss FM, na Smooth FM.
Ili kupata programu ya Songa Play, ipakue kutoka Play Store, App Store au Playapp, ingia kwa kutumia anwani yako ya barua pepe na jina la mtumiaji, na ufurahie vipindi vyako vya redio unavyovipenda, mix ya DJ na podikasti kutoka ulimwenguni kote.
Huduma hiyo inapatikana pia kwenye songaplay.com, App Store na Songa Playapp kwenye Play Store (Android).
Unaweza pia kutembelea www.songaplay.com kusikiliza moja kwa moja.
Songa Play pia hukuruhusu kutafuta podikasti; usipoipata, italetwa ndani ya saa 24.
Mtu anaweza kufikia programu ya Songa Play kutoka Kenya na duniani kote.
Unaweza kuiweka bluetooth kwenye gari lako au headphones kichwani ili kusikiliza unapoendelea na safari yako.
Unaweza kuingia kila wakati na kuendelea pale ulipoachia