WANASOSHOLAITI Vera Sidika na Huddah Monroe wameanzisha upya bifu lao kwenye mitandao ya kijamii kisa kuhusika katika uigizaji wa filamu za kihalisia.
Zogo hilo lilianza pale Huddah Monroe alipotoa maoni
yake kuhusu wanasosholaiti kuigiza katika shoo za kiuhalisia kwenye runinga.
Mfanyibiashara huyo wa bidhaa za urembo aliashiria
kwamba yeye hawezi kuigiza kwenye filamu hizo za kiuhalisia kwani kulingana na
yeye, shoo hizo haziongezi chochote cha mno katika maisha ya mtu zaidi ya
maigizo tu ya maisha feki.
“Ni
afadhali nitazame video za mbwa na paka kuliko kutazama shoo ya kiuhalisia au
simulizi ya maisha ya mtu kwenye vlog ya YouTube. Siwezi hata jitazama mimi
mwenyewe. Mkiwa wakweli, baada ya kutazama hizi shoo zote za uhalisia, ni vipi
ziliboresha maisha yenu? Kuna kitu mlijifunza? Zilikuwa na athari yoyote katika
maisha yenu?” Huddah alihoji.
Usemi huu ulioonekana kudunisha shoo za kiuhalisia
uliamusha popo za Vera Sidika ambaye amehusika katika shoo nyingi za
kiuhalisia, ya hivi karibuni ikiwa ile ya Real Housewives of Nairobi.
Sidika alicharuka kwenye Instagram na kumzomea vikali
Huddah Monroe ambapo alidai kwamba mwanasosholaiti huyo mwenzake huenda
anachukia shoo za kiuhalisia baada ya kukataliwa kuhusika katika moja miaka ya
nyuma.
“Jinsi
mtu Fulani anavyojitokeza akidai kuchukua shoo za kiuhalisia wakati alihusika
katika moja miaka 10 iliyopita ni ushetani. Ooh na alifukuzwa siku 5 baadae kwa
kufanya kazi duni. Kuhukumu watu kwa kutazama shoo za kiuhalisia si ukichaa
huo? Wakati ulikuwa kwenye moja ambayo ilikuendea mrama, hebu ifanye ieleweke,”
Vera Sidika alijibu mipigo.
Sidika aliendeleza manung’uniko yake kwa Huddah
Monroe akimshauri kwamba kama aliwahi kuhusika katika shoo ya kiuhalisia, hafai
kuwa hakimu kuwaamulia watu kama wanastahili kutazama au la.
‘Kama
umewahi kuhusika katika shoo ya kiuhalisia hufai kuwa mmoja wa kuwahukumu watu
kwa kuitazama. Wewe kunywa tu maji na ujishughulishe na mambo yako, haswa
wakati unajua kwamba ilikuendea kombo,” Sidika
aliongeza.
Tamko la Monroe linajiri wiki moja baada ya Netflix
kuachia msimu wa tatu wa Young, Famous and African, shoo ya kiuhalisia ambayo
inawahusisha mastaa katika sanaa ya burudani barani Afrika.