MWANASOSHOLAITI Vera Sidika amefichua kwamba yeye hata siku moja hujawahi badili dini kutoka Ukristo kwenda Uislamu.
Sidika
alifichua haya kwa shabiki mmoja ambaye alistaajabu kwamba kwa muda wote
amekuwa akifikiria kwamba Sidika ni Muislamu.
“Nilifikiria wewe ni Muislamu Vera,” shabiki alimuuliza.
Vera
alimjibu akisema kwamba maisha yake yote tangu utotoni yamejikita katika
Ukristo na kufichua kuwa alianza kuenda kanisani tangu enzi za mafunzo ya
watoto Jumapili kanisani.
“Ulisikia wapi? Maisha yangu yamekuwa
ya kanisani tangu siku za Sunday School,” Vera Sidika alisema.
Hata
hivyo, alifichua kwamba miaka kumi iliyopita, shetani alimrubuni na kufanikiwa kuondoka
maisha yake katika mkondo wa kanisani lakini pia akafichua kuwa katika siku za
hivi karibuni amekuwa akipiga hatua za kipekee katika kuyarudisha maisha yake
kanisani.
“Ni mpaka miaka kumi iliyopita wakati
shetani alifanikiwa kuniondoa kanisani lakini mimi ni Mkristo 1000%. Ni vile tu
sijakuwa nikienda kanisani kwa muda sasa japo katika siku za hivi karibuni
nimekuwa nikifanya juhudi za kurekebisha uhusiano wangu na Mungu,’ alisema.
Hii si
mara ya kwanza kwa mama huyo wa watoto wawili kuzungumzia kuhusu maisha yake na
jinsi alipotoka kutoka njia ya kuenda kanisani.
Mapema
mwaka jana, Sidika aliomba mashabiki wake ushauri wa kanisa ambalo lingemfaa
kwa ibada za kila Jumapili, akidokeza kwamba alikuwa na nia ya kumrudia Mungu.
Mwaka huu wa 2024 ninataka kujenga uhusiano mwema na
Mungu, sijawahi kuenda kanisani kwa muda sasa, mimi ni muumini, namuomba Mungu
na kufanya upande wangu kama Mkristo. Lakini inniwia vigumu kwenda kanisani.
Watu wananiangalia sana. Kunaye mmoja wenu ambaye anajua kanisa zuri ambalo
sitoweza kusumbuliwa na kuangaliwa, tafadhali pendekeza moja,” Vera Sidika aliomba.
Mwishoni mwa 2024, Sidika alichapisha video akiwa kanisani na
kuonyesha furaha yake kumaliza mwaka kwa kutimiza ahadi yake ya kuanza kumsaka
Mungu.
“Jumapili hii iliyopita ilikuwa mara yangu ya kwanza
kanisani kwa zaidi ya miaka 10 shukrani kwa BFF wangu @dyna_muthoni. Ilikuwa
azimio yangu ya mwaka mpya lakini shetani aliijaribu kwa miezi 10. Kila mara
‘nilisema nitaanza Jumapili hii’ haikuwahi kutokea. King’s house ni kanisa
nzuri kweli,” aliandika.