CROSSDRESSER maarufu kutoka Nigeria, Okuneye Idris Olarenwaju maarufu kama Bobrisky amezua mjadala mpya baada ya kukiri kwamba aliwahi kumpa mwanamke mimba wakiwa chuoni kabla ya kubadili jinsia kupitia msururu wa upasuaji.
Bobrisky alitoa ungamo hilo wakati wa
kipindi cha moja kwa moja cha maswali na majibu na mashabiki wake kupitia
Instagram.
Bobrisky alidai kwamba kabla ya tukio
hilo na mrembo aliyemtaja kwa jina moja tu – Lamide, yeye bado alikuwa bikira
na mrembo huyo ndiye alimvunja ubikira wake.
Mwanamume huyo anayejitambulisha kama
mwanamke pia alidai kwamba Lamide huyo ndiye aliyemtongoza wakiwa chuoni kwenye
bweni katika chuo cha Lagos.
“Kwa hiyo usiku ule tulikuwa
tukisubiri nani atagusana kwanza, mimi nilikuwa nimeegemea
ukuta, alikuwa akinikabili. Kwa sababu nilikuwa na haya, sikujua nianzie wapi,
sikujua la kufanya. Alianza kunishikashika na hatimaye tukafanya hivyo, hiyo
ilikuwa mara yangu ya kwanza na pekee nilikuwa na mwanamke,” alisema.
Bobrisky, ambaye alikuwa katika mwaka wake
wa pili katika chuo kikuu wakati huo, alikumbuka maoni yake wakati Lamide
alipomwangazia habari juu ya Siku ya Wapendanao.
"Haikuwa hadi miezi miwili au
mitatu baadaye. Siku hiyo ilikuwa hata Siku ya wapendanao. Kwa hiyo
alininunulia singlendi, chupi na takrima nilizohitaji shuleni. Sasa alikuwa
kama 'Bob mimi ni mjamzito Na nilikuwa kama' mjamzito vipi? Ulifanyaje? Shangazi
mimi ni mvulana mdogo sana, nimeingia tu 200 level. Tafadhali usiharibu maisha
yangu’,” alisimulia.
Alikiri kwamba alimwomba Lamide kuzingatia
"suluhisho" kwani hakuwa tayari kuwa baba wakati huo.
“Kisha nikamwambia tunahitaji
kutafuta suluhu kwa sababu sikuwa tayari. Alijua mimi ni mwanamke kidogo lakini
sio mwanamke huyu. Sijui labda alinipenda kwa sababu nilikuwa mwanamke,
sikuweza kujua."
Hata hivyo, Lamide alikataa na baadaye
kumripoti kwa kundi la wavulana, ambao walikabiliana naye kuhusu hali hiyo.
"Alisisitiza kwamba angezaa na
akaanza kunitukana, akanitoa wa kike na mimi pia nikaanza kumtupia
matusi," alisema.
Hii si mara
ya kwanza kwa Bobrisky kuzua kauli za kuchanganya wafuasi wake.
Mwaka jana,
alizua maoni kinzani alipodai kwamba ameanza kuona hedhi yake ya kila mwezi
baada ya kukamilisha upasuaji wa kubadili jinsia kabisa.
Aliwahurumia
wanawake ‘wenzake’ akisema kwamba hakuwa anajua hedhi huja na uchungu kiasi
hicho lakini akasema kwamba alikuwa tayari kukabiliana na changamoto mpya ya
kuwa mwanamke.