RAPA King Kaka amebaki kinywa wazi baada ya kuyakuta yasiyoweza kusemeka kwenye mtandao wa TikTok.
Msanii huyo ambaye waliachana na
mkewe mwishoni mwa mwaka jana alishangaa baada ya shabiki wa kike kujitokeza
kimasomaso akimtaka kumpa mimba.
Kilichomshangaza zaidi ni kwamba huyo
shabiki alimpa masharti ya kumpa mimba na kisha baadae aikatae endapo
atamtafute kumjulisha kuhusu mimba yake.
“King Kaka kuja unipe mimba halafu
uiruke,” Shabiki huyo kwa jina Ezna alimrai Msanii huyo.
Baada ya kupatana na maoni hayo
miongoni mwa watu zaidi ya elfu 12 kwenye kipindi cha moja kwa moja katika
ukurasa wake wa TikTok, King Kaka alibaki akishangaa na kusema ‘wuueh’.
Alipochapisha maoni hayo kwenye
ukurasa wake wa Instagram, watu walitoa maoni baadhi wakimshauri kumfanyia haki
Ezna na wengine wakisema kwamba hu oni mtego.
Haya hapa ndio maoni ya baadhi ya
watu kwenye ukurasa wake wa Instagram;
@khoerose8: “Lakini King Kaka huwa ni
mali safi tuseme ukweli tu.”
@_j.o.j.i_: “Anadhani utaruka juu
wewe ni sungura.”
@_.jokul_: “Hivyo ndio wao husema
halafu baadae unakuwa baba asiyetoa msaada katika malezi.”
@mona_binti_ali: “Wacha watakuanika
huku mitandaoni kama baba aliyekufa.”
@sue_oduya: “Halafu yeye ndio ataenda
kupea yule Obare chai eti wewe ni deadbeat.”
Maoni yak oni yepi kuhusu suala la
shabiki kumuomba msanii wake pendwa fadhila ya kupewa mimba?