logo

NOW ON AIR

Listen in Live

'Mapenzi studioni' na 'vitisho': Wafanyakazi wa Diddy wafichua tabia zake katika tasnia ya muziki

Kulikuwa na uhusiano wa kimapenzi mara kwa mara kati ya wafanyakazi na wanafunzi wa mafunzo, wanasema

image
na BBC NEWS

Burudani07 February 2025 - 10:15

Muhtasari


  •  Evans anasema jinsi anavyokumbuka vitisho alivyopewa na aliyekuwa mwajiri wake, Sean ''Diddy'' Combs- anayejulikana kama Puff Daddy kwa waliokuwa karibu naye.
  • Naye mfanyikazi wa kike anakumbuka alivyowahi kutumwa mipira ya kondomu amletee Combs akiwa kazini.

''Nina pesa nyingi hata naweza kukodi mtu akuue, na hakuna atakayejua.Hakuna atakayekufuatilia.Hutajulikana kabisa.''

Aliyekuwa mkurugenzi wa muziki Damiel Evans anasema jinsi anavyokumbuka vitisho alivyopewa na aliyekuwa mwajiri wake, Sean ''Diddy'' Combs- anayejulikana kama Puff Daddy kwa waliokuwa karibu naye.

Ilikuwa mwaka wa 1997, ambapo aliangushiwa tishio hilo katika ofisi ya New York

ya lebo ya muziki iliyoshinda Tuzo ya Grammy ya Combs ya Bad Boy Records.

"Ilikuwa kama, hivi ndivyo pesa inavyokufanyia," anasema.

Combs mara nyingi alikuwa "kama mwiba", lakini Evans anasema mamlaka yalikuwa yakimbadilisha.

Siku chache kabla, mwanahip-hop huyo alikuwa amepokea zawadi yake kubwa zaidi aliwahi kupokea tangu aanze muziki dola milioni 6 (£4.8m) kuashiria mafanikio ya lebo hiyo, ambayo ilijivunia wasanii wanaouza platinamu kama The Notorious B.I.G.

Mwaka huo kazi yake ya muziki ilikuwa imefika kileleni, himaya yake ikiendelea kutanuka na kuongezea fasheni, mvinyo na pia chumba chake cha televisheni.

Takriban miongo mitatu, urithi wake uko mashakani haswa akiwa amezuiliwa kwa jela akisubiri kusomewa mashtaka dhidi ya ke ya unyanyasaji wa kingono na msururu wa tuhuma za kutumia dawa za kulevya na vita katika sherehe zake za faragha, hoteli za kifahari na katika studio yake ya muziki.

Hata hivyo amekanusha tuhuma hizo zote.

Sasa BBC imezungumza na takriban watu 20 aliokuwa akifanya kazi nao katika studio yake chini ya rekodi yake ya Bad Boys -wakiwemo waliokuwa wakurugenzi, wasaidizi na wazalishaji muziki wakieleza wanavyokumbuka matukio ya kutamausha waliyoyapitiamikononi mwa Combs alipokuwa akiibuka kuwa maarufu miaka ya tisini.

Baadhi ya wakurugenzi wanasema walikuwa wakiingiwa na wasiwasi walipomuoana Combs akifanya ngono akiwa studioni, ikiwemo tukio ambalo mfanyikazi akisema aliwahi kuona mwanamke mchanga akiwa ofisini humo.

Naye mfanyikazi wa kike anakumbuka alivyowahi kutumwa mipira ya kondomu amletee Combs akiwa kazini.

BBC pia ilipata fununu kuwa fedha za kikazi zilitumika kusafirisha wanawake kote Marekani kwa ajili ya kufanya ngono naye pamoja na baadhi ya wafanyikazi.


Sean "Diddy" Combs, akiwa amevalia miwani ya jua na shati la buluu, akiwa amevalia hereni, nywele zilizonyolewa kimtindo, akiwa ameegemea meza ya studio yake ya kurekodia nyimbo, ambayo imetapakaa karatasi na kalamu za aina ya Sharpie.

Chanzo cha picha,Getty Images

Maelezo ya picha,Combs aliibuka kuwa milionea ghafla na uzinduzi wa Bad Boy Records mnamo 1993

Kulikuwa na tukio la kujirudia ambalo liliudhi tangu miaka ya tisini'' anasema Tony Buzbee, wakili wa Marekani anayewakilisha waathiriwa wa tuhuma dhid ya Combs, Ikiwemo mmoja anasema aliwahi kutishiwa maisha yake kama vile Evans alitanguliza kusimulia alichokisibu miaka ya nyuma.

Mwathiriwa anadai kuwa Combs alimdhulumu kingono akiwa bafuni katika tafrija zilizoandaliwa kwa The Notorious B.I.G., lebo yake kubwa ya nguli huyo wa muziki, mwaka wa 1995.

Baadaye anasema alitishiwa na Combs asiambie mtu kilichotokea la sivyo ''atapotezwa''.

Kupitia taarifa, mawakili wanaomwakilisja Comb wamemshutumu Buzbee kwa kupendelea kujitafutia umaarufu kupitia Televisheni bila ya kujali kusema ukweli na kumtetea nguli huyo wa muziki kuwa hajawahi ''kumdhulumu yeyote kingono'' au ''kusafirisha mtu pasi na hiari yake.''

Mawakili hao wanadai kuwa hawajapatiwa taarifa za kutosha kuhusiana na madai ya BBC ili kujibu madai hayo ambayo wanasema sio kweli.

''kamatulivyosema awali, Combs hawezi kuheshimu kila jambo la utangazaji au dai la kipuuzi kwa kujibu. Ana imani kamili katika mchakato wa mahakama, ambapo ukweli utatawala: shutuma hizi ni hadithi tupu," walisema mawakili wake.

Ukakamavu wake ulimfanya awe milionea ghafla baada ya kuzindua lebo ya Bad Boys Records mwaka 1993 akiwa na wasanii wachapa kazi.

Ilikuwa na kazi yake ya kwanza aliyejitosa, akiwa amejijengea jina kama mkurugenzi wa vipaji katika lebo tofauti inayojulikana kama Uptown Records akiwa na umri wa miaka 19.

''Alisema alitaka sana kuwa msanii tajika ulimwenguni na haikumkosesha raha iapo ungepinga au ungekubaliana na ndoto yake,'' anakumbuka Jimmy Maynes, aliyekwua mfanyikazi mwenza katika lebo aliyoanzia ya Uptown.

Maynes anakumbuka jinsi Combs alikuwa akijibeba akiwa kazini mara kwa mara alionekana kuwa na wasiwasi na kujikurupusha akiendelea na kazi yake.

Combs alifutwa kazi katika shirika hilo akiwa na miaka 23 na kuanzisha lebo yake ya Bad Boy Records.

''Ni mchapakazi na alipendelea watu wanaomzunguka wewe kama yeye,'' anasema Daniel Evans mkurugenzi mkuu ambaye alisimamia bajeti ya lebo ya Bad Boys records na kandarasi za wafanyikazi kuanzia miaka ya 1994 hadi 1997.

Combs alijielezea kama "mtu mwenye usasa" na alijulikana haraka kwa kukaribisha watu mashuhuri katika vilabu vya usiku vya New York, kwenye fuo za Cancun na Mexico

Hata Rais Donald Trump aliwahi kuhudhuria hafla yake katika miaka ya 90, anasema Evans, ambaye mara moja alimwona kwenye siku ya kuzaliwa ya kusherehekea miaka 30 ya Combs na akasema: "Mimi ndiye Mfalme halisi wa New York!"

Daniel Evans, a man with a shaved head and a graying beard, who wears a bright red jumper and a blue-and-white checked shirt, spotlit in a room with bare brick walls and large warehouse-style windows just visible in the darkened background

Daniel Evans, mwanamume mwenye ndevu za mvi, ambaye amevaa fulana nyekundu inayong'aa na shati ya rangi ya samawati na nyeupe, iliyotiwa madoa katika chumba kilicho na kuta tupu za matofali na madirisha makubwa ya mtindo wa ghala yanayoonekana tu katika mandharinyuma yenye giza.
Maelezo ya picha,Daniel Evans alisimamia bajeti za lebo hiyo na anasema fedha zilitumika kuwasafirisha wanawake kufanya ngono

Sote tulikuwa vijana sana. Mimi nilikuwa na miaka 24," anasema Evans, ambaye alikuwa mmoja wa wafanyakazi wa awali wa lebo hiyo. "Watu walitaka kujibarizi, kufurahi, kuungana na kujenga kumbukumbu nzuri."

Lakini akitazama nyuma, Evans anasema anahuzunishwa na baadhi ya mambo aliyoshuhudia kuhusu tabia ya bosi wake na utamaduni wa kampuni.

Kama mwaka 1995, anasema alikuta Combs akifanya ngono na msichana mchanga katika Studio ya Daddy's House, studio ya kurekodi ya Bad Boy huko New York karibu na Times Square.

"Nilikuwa nikijiandaa kwenda nyumbani usiku na kutafuta koti langu. Nilifungua mlango na akawa anafanya ngono na msichana huyu," anasema Evans, ambaye alidhani studio ilikuwa tupu kwa sababu ilikuwa kimya. Combs alilaani na kumshutumu kuondoka. "Nilidhani ntaachishwa kazi," anasema.

Anasema haikuonekana kuwa jambo la kushangaza wakati huo.

Lakini akikumbuka jinsi msichana huyo alivyokuwa kimya alipoingia chumbani, anasema: "Nikiangalia ninachojua sasa, kuna utata mwingi kuhusu hali aliyokuwa nayo… kwa kawaida, pande zote mbili huwa zinajibu sana wakati wa tendo."

Sherehe ya White Party katika Hamptons katika jimbo la New York, inayoonekana kutoka mahali pa juu, ikionyesha umati mkubwa wa watu wote wamevaa nguo nyeupe, wamesimama karibu na bwawa kubwa la kuogelea, ambalo lina daraja jeupe lililojengwa juu yake. Vigogo na matawi ya miti yamefunikwa kwa taa kubwa za pendenti za ulimwengu zikining'inia

Chanzo cha picha,Getty Images

Maelezo ya picha,Watu mashuhuri walihudhuria sherehe zilizoandaliwa na Combs wakiwa wamevalia sare ya nguo nyeupe lakini inadaiwa ufuska ulikithiri

Felicia Newsome, meneja wa studio ya Daddy's House kati ya mwaka wa 1994 na 2000, anasema kwamba tabia isiyofaa katika sekta ya muziki kwa ujumla ilikuwa inajitokeza sana wakati huo.

"Ilikuwa sio ya kawaida kama mtu aliripoti, lakini haikuwa ya ajabu kwa kuwa ilikuwa ikifanyika," anasema.

Newsome anasema mfanyakazi alikuita studio usiku wa manane akimkuta Combs amevaa chupi tu, akiwa na lengo la kufanya ngono na mwanamke mwingine. Alihitaji mfanyakazi huyo amletee kondomu, anakumbuka.

"Nikamwambia Puffy, usiwahi kumwambia mtu mwingine hapa akuletee kondomu," anasema Newsome.

Wakati mmoja, studio ilipoanza mwaka 1995, anasema Combs alikasirishwa na muonekano wa viti vya vilivyokuwa na muundo wa kizingiti cha juu na alimkosea heshima mbele ya wafanyakazi.

Anasema alimtaka aombe msamaha hadharani na kufunga studio kwa muda, akimwambia: "Kama mimi ninawaleta wanawake ofisi hii ambayo iko wazi masaa 24, unataka wakuchukulie vipi?"

Wafanyakazi wa zamani wanasema lebo hiyo ilikuwa inasimamiwa na wakurugenzi wa miaka ishirini na wengi wa wafanyakazi walikuwa ni wasomi, baadhi yao wakiwa bado wanasoma.

Kulikuwa na uhusiano wa kimapenzi mara kwa mara kati ya wafanyakazi na wanafunzi wa mafunzo, wanasema.

Evans anakumbuka tukio lisilo la kustahi na msichana wa miaka 14 kutoka timu yake, ambaye anasema alijaribu kumshawishi kingono.

Picha ya zamani ya rangi iliyochanganuliwa kutoka kwa jalada la korti, ambayo inaonekana ikimuonyesha Sean Combs kwenye studio yake karibu na ubao wa kuchanganyia muziki, akionyesha ishara kwa mikono miwili kwenye kamera, na mwanamke mchanga amempakata. Uso wa mwanamke umefichwa.

Chanzo cha picha,Handout

Maelezo ya picha,Moja ya mashtaka inasema picha hii inamuonyesha Combs akiwa studio kwake akiwa na mtoto wa miaka 17 ambaye anadai kuwa alimbaka

Wasanii na wafanyakazi wengine katika lebo ya Combs wangeweza pia kuomba wanawake kuletwa kwa ajili ya kufanya ngono studioni, anasema mkurugenzi wa zamani.

"Kama walikuwa na umahiri wa ngono, wangeletwa," anasema Evans, ambaye alisema alijua kwa sababu alidhibiti bajeti. Pesa kwa ajili ya ndege zilikuwa zikitengwa na kuorodheshwa chini ya gharam ya safari, anaongeza.

"Labda ilikuwa kama maelfu ya dola," anasema Evans. "Sidhani kama ilikuwa inatokea mara nyingi, lakini ilikuwa ni gharama ya kurekodi."

Evans anasema maombi ya Combs yalikuwa yanashughulikiwa na wasaidizi wake binafsi.

Mmoja aliiambia BBC kwamba Combs alijua kuwa aliwaambia kuleta wanawake aliokuwa "akichumbiana nao" na kuwafadhili kwenye hoteli, ingawa msaidizi huyo alisema hawakuwa wafanyakazi wa ngono.

Katika miaka ya 2000, studio ya Daddy's House ilibadilika zaidi, wanasema wafanyakazi wawili wa zamani, ikawa na utamaduni wa "ngono, dawa za kulevya na tafrija zisizokwisha."

Studio hiyo ni mojawapo ya maeneo ambayo wanawake wamekuwa wakimshutumu Combs kwa kuwaekea dawa za kulevya na kuwadhulumu kimapenzi.

Mwanamitindo Crystal McKinney anadai kuwa tajiri huyo alikunywa naye pombe na bangi kabla ya kumdhulumu kimapenzi mwaka 2003.

Mwaka huo huo, mwanamke mmoja anadai kuwa Combs na wenzake wawili walimdhulumu kimapenzi katika studio wakati alikuwa na miaka 17.

Mawakili wa Combs wanasema anangojea kuthibitisha kutokuwa na hatia, wakiongeza kuwa madai ya McKinney hayana msingi.

Takriban majasusi watano wa Uchunguzi wa Usalama wa Nchi wanasimama kwenye barabara usiku huko Miami, wakimulikwa na taa za gari aina ya SUV   inayoonekana kuwa ya maafisa wa polisi. Mmoja wa mawakala, ambaye anaongoza mbwa wa polisi, amevaa miwani.

Chanzo cha picha,Getty Images

Maelezo ya picha,Nyumba za Combs - ikiwa ni pamoja na hii ya huko Miami - zilivamiwa mwaka jana kama sehemu ya uchunguzi wa biashara ya ngono

Wengi wa wafanyakazi wa zamani wanasema bado wanapata shida kuhusisha shutuma hizo na mtu waliemjua.

"Haya madai ni ya kushangaza kwangu, kama ilivyo kwa wengi katika kikosi chetu," anasema Jeffery Walker, rafiki wa karibu wa Combs ambaye alikuwa sehemu ya timu ya uzalishaji ya lebo ya Bad Boy.

"Nimeenda katika tafrija hizo na bila shaka kwenye vikao vya studio, na hakuna chochote kilichodaiwa kufanyika mbele ya macho yangu."

Evans pia alikuwa na shaka kuhusu baadhi ya madai hadi aliona video ya Casandra Ventura, mpenzi wa zamani wa Combs kwa miaka kumi na msanii wa zamani wa Bad Boy, akipigwa vikali na msanii huyo wa kufoka katika hoteli huko Los Angeles mwaka 2016.

Ventura alikuwa mtu wa kwanza kumshutumu Combs mnamo Novemba 2023, akidai kuwa alimnyanyasa kingono wakati wa uhusiano wao. Combs alikubaliana na kesi hiyo siku iliyofuata na kumlipa pesa kiasi kisichojulikana.

"Sio mara ya kwanza kuona hasira hiyo," anakumbuka Evans, akirejelea tishio la kifo aliloshuhudia mwaka 1997. "Ni vigumu kuona. Mtu aliye kwenye video na Cassie ni kama yule ambaye alimtishia mfanyakazi. Kwa hiyo, unajiuliza, je, kuna kilichobadilika?"

Kwa miaka mingi, Sean Combs amebadilisha jina lake mara kwa mara - kutoka Puff Daddy, hadi P Diddy na katika miaka ya hivi karibuni, "Love."

Kwa maelezo zaidi yatakayojitokeza atakapofikishwa mahakamani kujibu kesi dhidi yake katika mwezi wa Mei, wengi wa wale waliokuwa karibu na nguli huyo wa muziki wanajiuliza kama walimjua Sean Combs kikamilifu.

"Mtu anaweza kufikiria kuwa yeye ni mtu mchafu, lakini hiyo siyo kumbukumbu yangu ya Puff," anasema Jimmy Maynes, aliyelelewa na Combs huko Mount Vernon, New York.

Lakini baada ya kupumzika, anaongeza: "Au labda pesa inawapa watu uhuru wa kuwa katika tabia zao halisi, na alikuwa mtu huyo kila wakati."


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved