MWANAMUME ambaye anajipiga kifua kwa kuwa na familia pana yenye wake halali wawili na wanawake wengine 5 ambao amezalisha nje ya ndoa amedai kwamba yuko tayari kuendeleza msururu wake wa kuzalisha wanawake tofauti tofauti.
Mwanamume huyo mwenye umri wa makamo alikiri hayo wakati
alipotokea kwenye mahojiano ya runinga.
Alisema kwamba yeye hupata tulizo la moyo katika kumpa
mwanamke mimba pindi anapohisi kuwa na msongo wa mawazo kutokana na mahusiano
na wanawake wengine.
“Mimi nina wanawake
wawili, pia nimezaa nje na wanawake 5 hivyo kwa jumla nina watoto 7 kutoka kwa
wanawake 7. Na katika hawa wanawake wangu wawili, mmoja ni mzungu mwingine ni
mwafrika. Na wote tumeoana kwa njia halali kabisa kwa neema ya Mungu,” Mwanamume huyo alieleza
kwa majigambo tumbi nzima.
“Sasa, sharti nambari moja katika nyumba yangu ni kwamba kama watanipa msongo wa mawazo kupita kiasi hiyo inamaanisha ni lazima nitoke nitafute mwanamke mwingine, kwa sababu naamini ninaishi mara moja tu!” aliongeza.
Video hiyo ambayo ilichapishwa kwenye ukurasa wa Facebook kwa
jina 9ja Now ilivutia maoni mseto, baadhi wakimuunga mkono kwa dhana kwamba
anafurahia maisha yake duniani huku wengine wakidai kwamba alikuwa anawachezea
wanawake shere.
Wengine pia walimkosoa kwa kurasmisha uchepukaji katika ndoa
kuonekana kama jambo la kawaida licha ya kuwepo kwa magonjwa ya zinaa mengi.
@Victoria Anene: Unaweza kufikiria. Mwanaume huyu anadhani
anawafanyia wanawake upendeleo.
@Paul Mgbameh: Wewe ni mtu asiyewajibika sana.