Mwanamuziki wa kiker aia wa Tanzania Gift Stanford Joshua ambaye anajulikana kwa jina lake la muziki Gigy Money amefunguka kwamba anatamani ndoa kwa vyovyote vile.
Kwa upande wake anasema yuko tayari kuingia katika ndoa bila kujali mahari atakayotoa mumewe. Pia anakiri kwamba anaamini sana kwenye mapenzi.
"Mimi niko na roho ngumu, mimi ata nikipata mwanaume muisilamu naolewa, yaani bora awe mwanaume, kama ng'ombe ndo tunakula tunakufa. Ata elfu moja. Mimi naamini kwenye mapenzi Hamisa sai amependa Azizi, watu wengi hawakwaamini hilo penzi liko. mimi naumia natamani ndoa yenye Penzi," mwanadada Money alieleza.
Mwanamke huyo Gigy Money aliwahi kudaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki wa Tanzania Ali Kiba, ila Kiba kwa upande wake alikanusha madai hayo kutoka kwa vixen huyo.
Gigy Aliwahi kutoa kauli kwa umma kuhusu matamanio yake ya kupata watoto na mwimbaji maarufu wa bongo, rais wa Wasafi Diamond Platnumz na vilevile mtangazaji wa runinga ya Tanzania, Idris Sultan.
Mnamo mwaka 2020, Gigy Money alikuwa na mapigano makali na mpenzi wake wa wakati huo ambaye alikuwa mzaliwa wa Nigeria kwa jina la utani Hunchy Huncho ambao walitengana baada ya tukio hilo.
Gigy Money pia aliwahi kudai kuwa na idadi kubwa ya utoaji mimba ila bado alifanikiwa kupata binti aliyempata na mpenzi wake wa zamani.
Mwanamziki huyo mara kwa mara ametuhumiwa, kushtakiwa na wakati mwingine kupigwa marufuku kwa kukiuka utaratibu wa uendeshaji wa shughuli za sanaa nchini Tanzania.
Hili hasa limechangiwa pakubwa kwa kutumia lugha chafu na kuchapisha maudhui ya uchi kwenye mitandao yake ya kijamii.
Mwaka 2019 Baraza la Sanaa nchini Tanzania lilimpiga marufuku Gigy Money kufanya shughuli zozote za sanaa ndani na nje ya Tanzania kwa muda wa miezi sita na kutoa kiasi cha shilingi milioni moja za Kitanzania kwa kosa la kudhalilisha utu wake.
Aliadhibiwa, kisa alitumbuiza akiwa amevalia mavazi yaliyoonyesha mwili wake nusu uchi katika tamasha lililorushwa moja kwa moja kwenye runinga ya Wasafi ambayo pia ilipokea adhabu ya miezi sita kutoka kwa mamlaka ya Mawasiliano ya Tanzania kufuatia tukio hilo.