MTUMIZI mmoja wa mtandao wa X amejitolea kumsaidia muuzaji wa magari Khalif Kairo kwa usafiri katika kipindi cha miezi mitatu.
Polo Kimani, kupitia jukwaa la X
alichapisha ujumbe akitoa ahadi hiyo kwa muuzaji huyo wa magari ambaye mwaka
huu ulimuanzia vibaya biashara yake kuporomoka lakini pia kuwa mgeni wa vyombo
vya dola mara kadhaa.
Kimani alisema kwamba kwa vile Kairo kwa
sasa yuko kwenye matatizo mengi, yeye kama rafiki yake amejitolea kumsaidia na ‘lift’
kila siku Kwenda kazini kwa kipindi cha miezi 3 ijayo.
Hata hivyo, msaada wa Kimani hautakuja
rahisi hivyo, alisema kwamba kama Kairo atahitaji kuaidiwa na ‘lift’ kila siku
kwa miezi 3, asi sharti atii masharti yake ya kutokea kwa Barabara alfajiri ya
saa moja kasoro dakika 10 kila siku ili kumsubiri amchukue.
Kimani alisema kwamba Kairo ikiwa anahitaji
hiyo ‘lift’ yake, basi itabidi anatokea kwa Barabara anayopita na gari lake
alfajiri hiyo akimsubiri.
“Nina furaha kumpa kairo lifti kwenda kazini kwa miezi 3 ijayo bila malipo,Bora 6:50am ikue inampata kwa lami ameningojea,” Polo Kimani alisema.
Aliendelea kumpa Kairo masharti zaidi
akisema kwamba ni lazima akubali kuketi katika viti vya nyuma na bila kuongea
chochote hadi afikishwe kazini kwake.
“Itabidi amekaa nyuma juu mbele ni
kwa bibi,pia yeye nampeleka kazi,” Kimani
aliongeza.
Hata hivyo, baadhi walimtania kwamba hiyo
itakuwa ni kumkosea Kairo heshima ikizingatiwa kwamba mfanyibiashara huyo
alikuwa mwenye Maisha ya kifahari mwaka jana.
Walimtania kwamba Kairo nim tu ambaye
alikuwa amezoea Maisha ya gari la kifahari aina ya Porsche Cayenne na kwamba
itamkalia vigumu kuabiri gari lolote lenye haiba chini ya Porsche.
Haya hapa baadhi ya maoni ya watumizi wa X
kwenye chapisho hilo;
@wa_ngachu: Uko sure gari Yako itafika
standards alikuwa ameset za Porsche cayenne kwanza Ile ya kupenda reggae music
alafu ujue anapenda kutumia express way.
@snrgoodman: Huyu ni kijana wa cayenne
mnapea ultimatum 😂😂😂
@nyuki6634: Kumbe pia wewe kairo
alikusaidia ukanunuwa gari na huwa hamsemi 😂